Asali ni zaidi ya utajiri

Jamasa upo sahihi eti wewe unaetoa mzigo ndio unabanwa wakati mzigo ulitakiwa wabane wale wanaohitaji kwamba tunahitaji wa kiwango hiki sema wengi sio Wafanyabiashara hasa watunga sheria ndio maana wanaona bora iwepo tuu Tanzania wakati kuna Nchi hiyo asali kidogo tuu huwezi kuigusa kwa bei yake na ya kawaida tu sasa nyingi inaenda Kenya,Rwanda na kwingineko kwa ajili ya kuuza Nchi zilizoendelea...
 
Sasa ndugu. Hapo utajiri uko wapi. Sema ukufanya hato unajiongezea kipato. Hizo shughuli za shambani zingekuwa hivyo vyombo vya anasa vingehamia huko. Hakuna shughuli ya kilimo na ufugaji ndogo. Sema watu wafuge nyuki wajiongezee kipato kama kipo kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inabidi wenye mamlaka walifanyie kazi hili jambo maana wachina mpaka sasa wana pata pesa nyingi za kigeni kwa kuweka uhuru wa ku export
***
 
Mzee baba hunitakii mema , hapo juu nimepost sample ya biashara yangu soo hapa nikifunguka tuu jua na posibility ya 98% ya kupatikana na kupewa kesi ya uhujumu uchumi ama uchochozi, vizur tuishie hapo tuu for the sake of my peace.

***
Nimekuelewa chief make unaweza kuwa blackmailed na mwendesha mashtaka wa Serikali ,.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Thanks bro,nina jirani yangu hapa Mwanza alilima miti mingi kama hekali 5 hivi,tuseme ana msitu tena katikati ya makazi ya watu,
Nataka niingie ubia nae niweke kilimo cha nyuki sasa sijui kitapata tija kwa maeneo ya hapa mwanza au najichanganya?
Naomba msaada wa ushauri wako na wa wadai make napenda kilimo hichi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wadau

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Barikiwa sana ....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashauri wajasiriamali wawe proactive. Inawezekana sheria na kanuni zilizopo zimepitwa na wakati. Baadala ya kulalamika, wadau waorodheshe vizuizi na mapungufu katika hatua zote mpaka mzigo unaposafirishwa nje na mdau kulipwa. Itapendeza kama kutakuwa na ulinganifu na nchi nyingine za jirani.
Basi waraka kuomba mabadiliko ili kuifanya sekta 'export friendly' na kuna win-win situation ungewasilishwa serikalini au kupitia wabunge. Mbona sekta ina mdau mkubwa aliyehamasisha sana ufugaji wa nyuki ambaye kwa sasa ni waziri mkuu mstaafu.Kwa nini hamfikirii kumtumia huyu kuiinua sekta?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwenye biashara changamoto ya competitor wako ndo fursa yako ya kujitanua na kujikuza kibiashara na ndo faida inapo patikana kubwaa,

naamini yeye mwenyew anajua hizo process za ku export lakin yeye sio mjasiriamali bali ni muwekezaji, anaweza kununua mashine za kisasa na kuprocess asali kwa kiwango cha kimataifa kabisa,

Na akiwa alone kwenye issue ya kuexport anatawala masoko mengi na kwa gharama anazo zipanga yeye, akisema atusaidie na sisi wadogo atakua ana jipalilia moto, ndo wengi wanavyo fikiria ivo.

Lakini waziri mkuu alikaa na wafanya biashara na walimwambia kuhusu TFDA, TBS na wengine wengi ambao majukumu yao yanafanana na wamekua kwenye kazi izo kwa kukwamisha biashara za watu tuu kwa kutaka rushwa,

mwarubaini wao ukipatikana itakua ni good start ya hizo vipengele vingine vya export.

***
 
Dawa ya uchumi kulegaleaga iko hapo!

Tuna nature products nyingi sana zinazohitaji kuongezewa thamani kidogo tu ili ku conform na Export Standards. Ila kwa nchi ya kipuuzi inafikiri kuwakaba koo matajiri ndio kuimarisha uchumi.

Vitu vya maana kama hivi havizungumziwi kabisa, na wachumi wapo kibao wenye Ma CV makubwa tu. Wao wakila wakashiba na familia zao ngonjera zinazosalia ni uchumi wetu umeimarika, wengine vijana mjiajiri.
 
Bora nikalime vitunguu saumu,asali kuisafirisha inamlolongo mkubwa kama pembe za ndovu,labda kandoo kako moja kama unatoka safari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…