Asante Azam TV mmeleta uhalisia

Mingendeu

Senior Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
115
Reaction score
237
Simba na Yanga hiyo kabla ya Azam TV.

Radio kubwa ya kaseti mbili ya Mzee Mahira imewekwa barazani. Wengine tumesimama, wengine wamekaa. Tumejaa kibaoo. Hii ndo ile mtoto hatumwi dukani.

Hapo inaweza kupigwa mbungi DK 5 na usisikie jina la mchezaji.

Utasikia inapigwa kulia kule kwa jezi nambari 7, inatupwa kushoto kwa jezi nambari 11 anapiga chenga moja hatari pale, kuna mtu kalamba nyasi kule nani yule?? πŸ˜‚πŸ˜‚ amedanganywa Kama anapewa vileee -akakubali, akajiandaa kuichukua -kumbe alishachelewa matokeo yake katereza vibaya mno

"Anapita vizuri pale anamtafuta Suleiman Matola, Matola anakokota mpira haoni mtu, analalamika pale"

Matola anacheza fyongo amepokonywa mpira imepigwa ndefu hadi katikati ya uwanja, kuna kitu kinaendelea hapa sijui ni nini kimetokea, lakini mchezaji mmoja yupo chini. Refa nae hajui nini kimetokea anasema kabumbu lipigwe.

(Muda huo umati upo kimyaaaaa unasikilizia redioni)

Ally Mayai anaichukua vizuri ile, anaipiga pasi inatembea Kama nyoka. Inachukuliwa na Edibily Lunyamila, Lunyamila na mpira anakutana na konga la jezi namba 20 kibaba kwelikweli, kimetitia hatari, ilikuwa rafu mbaya sana lakini refa anapeta. Wachezaji wa yanga wanalalama pale, refa anasema huu ni mpira wa miguu, ni mchezo wa kugusana, Kama huwez kacheze draft.

Kabumbu lipo upande w simba sasa, Bakari Malima bado analalamika hapa. Salvatory Edward anasema cheza mpira.

(Huku tuliopo nyumbani radio "refa simba huyu")

Mtangazaji : Mama weeee, jezi nambari 10 yule anachomoka mbio za hatari hapa Go Gooo Goooooooooooooooooool halafu kimyaaaa

(Unasikia kelele za uwanjani) vigoma na kelele za mashabiki

(Huku kila mtu, kimyaaaa. Anataka kujua nani kafunga)

Mtangazaji: Ni jezi nambari kumi mgongoni Iddi Moshi yule.

(Washabiki wa Yanga wanashangilia)

Mtangazajj: Alichomoka vizuri akapiga shuti Kali, iligusa nyavu ndogo za nje. Ni goal kick. Huu ni uchawi, unakosaje paleπŸ˜‚πŸ˜‚

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ watu tunaosikia redioni ( aaaah Simba wachawi Sana, ngoma imeingia kabisa , Ila na refa anawabeba sana)
 
Ashukuruwe aligundua teckonolojia mkuu ,,haiongopiiii
 
Kwa nini usiseme ITV? ITV imetangulia muda mrefu tu inaonesha mpira mubashara, ikaja TVT/TBC tukawa tunatazama mpira mbashara, in the late ikaja azam tv, ikawa ina host ligi kwa mkataba wa kuonesha live mpaka sasa ni azam tv ndio yenye haki ya kurusha matangazo ya mpira ligi kuu peke yake, tv zingine za mwanzo hazioneshi mubashara hazina haki ya kurusha
 
Ni kweli lakini jaribu kulinganisha zile picha za mechi za ligi za TVT na Azam. TBC ya Leo huwa wanarusha baadh ya mechi hasa za timu ya Taifa lakini ubora bado wanajikongoja.

Azam wamekuja na technolojia kubwa kiasi.
 
Dah ile ya gold kufungwa mtangazaji kimya ina mzukaaa utasikia ooh shamanic adobe kataka kuisola imwana imwana nae kalemwa kalemwa miguu cabana kwa uchungu ohhhjj ohhh kidedea ohhh ohhh didedea au yanga utasikia yanga yanga yanga yanga halafu ccm ccm ccm
 
Hatari sanaπŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…