Asante jkt umetuonyesha udhaifu wetu

Joined
Aug 28, 2013
Posts
33
Reaction score
4
Najua utajiuliza y nimeishukuru JKT, nimeishukuru JKT kwasababu baada ya JKT kuona wanafunzi wanstahili kwenda chuo ikasema wanafunzi waandike barua na hapo ndipo udhaifu wetu ulipojitokeza, mpaka sasa nimeona vijana wengi wanahangaika hasa huku Mwanza na kuna jamaa yangu yupo Dar nae anasema hivyo kwamba vijana hawaelewi barua waandikeje, hapa ndipo linakuja swali inamaana vijana wetu hawajui kuandika barua au hawajaelewa waandike nini? Kiukweli nimekuta vijana wamekaa makundi wanajadili waiandike vp barua ili ieleweke, jamani rafiki barua hii ya JKT kwa mtazamo wangu haihitaji mbwembwe nyingi bt unaiandika kwa mpangilio mzuri wa barua ya kikazi na dhumuni lako usilifiche. Kumbukeni o Lvel mlipokuwa mnaandika barua za kikazi kwenye somo la kiswahili. Msituangushe jamani

ANGALIZO: Epukeni kuandika kiswanglish yaani unaandika kiswahili unachanganya na Kingereza na pia ni vyema ukaandika kwa kiswahili kuliko kuandika kwa Kingereza. Ni hayo tu kama unachaziada cha kuwaambia wadogo zetu funguka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…