Asante Kijana wetu Sabaya Umetusafishia Wilaya yetu. Tutakukumbuka kwa mema yako yote

Uchaguzi wa mkuu wa wilaya au?
 
Mwakibinga mimi nakuelewa maana ulikuwa mtu makini sana enzi tuko pale UDOM ulisimamia ukweli, lakini mwisho hakupata lolote uliishia kuwa loser.
Pole sana, sasa hivi umeamua kujikomba komba labda utapata chochote. Pole mwakibinga
Bado jamaa ana-loose tu, kwa mfano hapa anadandia meli ambayo imeshazama! Anamtetea Loser?! Labda anahisi ataenda jela soon, anataka akawe wake huko?!
 
Huyo Sabaya alikuwa anafanya nini madukani Arusha??
Kama alikuwa DC kwann asitumie plate number tuna za DC, badala yake anabandika DFP na UN?

Tuachane na Hai kwanza.
Huruma ya wananchi hatoipata, kwa sababu aliwaumiza wananchi hata tusioishi Hai, zile CCTV zilituonyesha unyanyasaji.
Sijawahi kuona DC atenguliwe au asimamishwe na watu wapombeke kama Sabaya.
Wa aina yake wajitafakari.

Everyday is Saturday............................ 😎
 
Kuna watu walilipwa hela nyingi Sana wamsaafishe BILIONEA SABAYA tatizo imeshindikana.Yule jamaa kawa BILIONEA kwa pesa za zulima.Ipo siku tutaweka ushahidi.na hapo ndo mtaumbika nyinyi watetea uovu.
Hakuna ushahidi wa mwamba kujimilikisha chama? Tuleteeni kama nahuo ushahidi mnao
 

Hii ndiyo kwa kiingereza inaitwa FALLACY. Dhana ya kipumbavu iliyoasisiwa na kushamirishwa na watu wasioelewa kabisa mantiki ya demokrasia ya vyama vingi vya siasa. Ni sifa ya kijinga mtu kutambulika kama “KIBOKO” ya kiongozi wa chama kikuu cha upinzani na mbunge wa jimbo toka chama cha upinzani kihivyo.

Mtu anatumia violence: kuteka, kutesa na kuharibu mali za wapinzani huku akilindwa na polisi na viongozi wa juu kitaifa. “Mwanasiasa” asiye na uwezo wa kushindana na wapinzani kwa hoja badala yake anategemea harakati za kijambazi akilindwa na polisi kuvuruga na kuhakikisha wapinzani hawafanyi kazi yao jimboni. Halafu huyo ndio athaminiwe kama “mfia chama” wa CCM? Eti kiboko ya Mbowe? Nonsense. Ni aibu kwa CCM leo hii kutegemea mbinu za kijambazi na watu aina ya Sabaya.

Bila mwendazake, Sabaya asingekuwa lolote wala chochote. PM, RC, polisi, walishindwa kumtuliza sababu ya JPM aliyekuwa akithamini “vichaa”.

Sasa kaishia kuwaaibisha wakuu wake kwenye Tv interview. Waliosema ukicheza na mbwa atakufuata hadi … hawakukosea. Kazi kwake HE SSH kama anataka kurejesha heshima ya CCM kama chama cha SIASA au cha KIFASHISTI kukamilisha mipango ya mwendazake JPM.
 
Bro naona unahangaika sana. Wewe ni Mwanaume bhana. Be a Man Common!!

Unajua unavyofanya hivyo haujengi bali unazidi kumuharibia Jamaa kwasababu inaonekana ni HARAKATI ZA SABAYA Mwenyewe.

Nadhani nyie ndio Mlimshauri akaenda Cloud TV kipindi hiki cha kujipanda upya kwa serikali. (Hamkumshauri vema).

Sasa naona unakuja na Kampeni za wazi kama vile unamshinikiza Mama.
 
Alafu bado unaandika maelezo mareeeeeeeeeeeeefu kumsifia. Wanasiasa mna tabu sana. Unaeleza mapungufu weeeeeee alafu unamalizia naunga mkono hoja
 
Kwa Kiriwe wametukwamisha sana siku 3 hizi, Sisi tusiokunywa pombe! Tungekunywa alkasusu pale kwa kusherekea Masai mbakaji kung’olewa!
 
Gerald Magembe alafu Hai iwe wilaya yako?
 
Hai ni wilaya iliyojaa ufisadi mkubwa ktk mkoa wa Kilimanjaro na ndo hao waliathirika Sana na mfumo uliopita.hai ina kundi la wafanyabiashara ambao kwao Kodi ni haramu na biashara halali kwao hailipi.Hai imewakamata vijana wengi wa kitz na kuwaaminisha kuwa wao wanadhulumiwa na mifumo.Hai kuna kila aina ya uozo,ufisadi,uzandiki unaofanywa na kikundi kidogo Cha mataikuni ambacho chenyewe kinataka kifanye kila kitu bila kuguswa bila kujali kinafuata Sheria au hakifuati Sheria na kakikundi haji ka watu wachache wa hai ndiko kwao sabaya alikuwa Kama adui mkubwa kwao ni kea sababu tu alisimamia utawala wa Sheria na haki.Hivyo yatasemwa mengi lkn ukweli kwa watu wanaofahamu utabaki Kama ulivyo.Shida ya watz wengi si mtu Bali ni watu ambao kwao binadamu si kitu Sana Bali Mali ndo msingi na kwao ni vigumu kuamini kuwa watu ndo chanzo Cha maisha yao.kwao hata Kama watu wakifa ni sawa lkn maisha yao yaendelee bila kuguswa.kwao maskini si kitu Bali wao ni kitu.hiyo ndo shida yao kubwa.
 
Hoja hujibiwa kwa hoja na si matusi na ukiona mtu anatukana huyo Hana hoja na kafirisika kiakili na kimawazo hivyo awaachia wenye akili timamu watoe hoja
 
Wewe umeona ukweli na huo ukweli utakuweka huru siku zote.umekubali kuachana na unafiki wa humu jamvini na umeamua kusema ukweli.hivi ndivyo tunapaswa kuwa na si kuaninishwa uchafu kuwa usafi.
 
Kweli USA maisha magumu..
umekubali kuufedhehesha utu wako kwa vipande vya fedha.

kakutumia ngapi hadi ukademka hivi, maana sabaya ni bilionea.!
 
Mimi ningekuwa wewe ningekaa kimya. Umeongeza nini kwenye CV yako zaidi ya kuharibu? Kutoongea sana ni werevu... Hususani unapotegemea Siasa kama kazi yako. Soma upepo bro.
 
Sasa Si chunguzi utasema Kama ana makosa Au laa? Mbona mnaweweseka Mataga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…