Asante M Zahera wewe ni zaidi ya kocha kwa Yanga

idawa

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Posts
25,284
Reaction score
38,364
Amsema Yanga sio maskini hadi kuwa ombaomba.
Amesema katika uchunguzi wake wa juujuu amegundua Yanga inamashabiki zaidi milioni 5, amesema mashabiki hao kila mmoja akichangia 2500 kwa mwezi ni zaidi ya bilioni 2.5 kwa mwezi , hivyo Yanga sio Maskini tena.

Amesema sasa hivi wanampango wa kufungua akaunti crb, signature atakuwa Yeye Zahera,Ajibu na Salehe kiongozi wa Uangalizi hivyo mashabiki msiwe na wasiwasi na pesa zenu.

Amesema sasa hivi yupo Studio na wachezaji 7 wakitengeneza tangazo litatoka wiki ijayo kuhamasisha mashabiki kuchangia timu yao...

Asante Zahera Mungu akubariki, ila kuna watu hawajapendezwa na kauli yako hivyo tegemea Majungu.
 
Hajaijua Bongo yetu huyu, angejikita kwenye kazi yake, huko anakoenda atajiharibia.
 
Halishindwa Manji kuchukua buku buku tu ,zilianzishwa kadi za bank ya posta
 
Hivi vilabu vikongwe vya Simba na Yanga ukiangalia idadi ya mashabiki walionao Tanzania wenye vipato vya kati na juu na jinsi mchezo wa soka unavyopendwa na Watanzania vikijipanga vyema vinaweza kuwa moja ya vilabu vya soka tajiri kwenye ukanda huu wa Africa Mashariki na tunajua jinsi pesa inavyoweza kuleta mafanikio kwenye klabu hasa michuano mikubwa kwa kusajili wachezaji wazuri sema ndio hivyo kupanga ni kuchagua.
 
Mkuu siku zote fanya unachoona sahihi. Huwezi sema atajiharibia ila watajiharibia wao wenyewe. We unavyoona anafanya kitu sahihi au sio sahihi?!

Anachofanya ni sahihi sana, ni kitu viongozi wa hizi timu wamekuwa wakishauriwa kukifanya muda mrefu.

Shida kubwa hizi timu zetu ni kugombea maslahi.
 
Yanga tunabahati
 
Dawa ya hizi timu ni kuwa kampuni au kuwa registered kujiendesha kibiashara, haya mambo ya kuchangishana ni wazo la kitoto halina future sana sana litaleta migogoro.. Kila mtu pale kaenda kutafuta pesa hata kocha anatafuta pesa kwa hiyo ni vizuri mambo yakaenda kwenye utaratibu na mkono wa sheria .. kama wanauza hisa waseme ni hisa siyo tu mtu kutuma buku sijui buku jero..


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…