kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Yanga ilicheza na Club Africain uwanja wa kwa Mkapa na kutoa sare ya bilabila. Kwa anaefahamu mpira huu ulikuwa ushindi mkubwa kwa Yanga, hata Club Africain wenyewe wanalitambua hili.
Cha kushangaza wachambuzi uchwara na Makolo wanataka kuwaaminisha watanzania, wapenzi na wadau wa Yanga wote kuwa Yanga ni dhaifu, wachezaji hawafai, kocha hafai na uongozi haufai kwa yanga kupata sare ya 0-0 kama kwamba hawajui kwamba hata Al-Hilal na Club Africain ni timu kubwa sana Afrika na wanastahili kufungwa tu Yanga. Anaeamini kwenye upuuzi kama huu sio mwanamichezo bali ni mshabiki maandazi au anatafuta ahueni ya timu yake kwa Prof. Nabi na benchi lake la ufundi kufukuzwa na kuitafutia Yanga migogoro.
Kama yuko mwanayanga anaeamini kuwa kwavyovyote vile Yanga inastahili kuzifunga timu zote za nje ya nchi mshabiki kama huyo ni mjinga na mbumbumbu wa michezo anaejifanya ana uchungu mkubwa na Yanga kuliko Eng. Hersi au GSM anaemimina fedha zake.
Nijuavyo mimi Club Africain sasa hivi wana wasiwasi mkubwa kuzidi ule walionao Yanga, kwakuwa wanajua hata sare kwao haiwafai na wanajua Yanga ina wachezaji ambao wanaweza kupata goli kwenye uwanja wowote ule duniani.
Tuache ujinga na mihemko, hakuna ubishi kuwa Nabi hapendwi na timu zoote kwenye ligi. Ni mtu mpumbavu tu ambae atamfukuza kocha ambae anashinda timu zote kwenye ligi huko akijua kuwa ili upate nafasi ya kucheza mashindano makubwa lazima kwanza ufanye vizuri kwenye ligi yako kwanza.