Asante Mungu Yanga haikufungwa nyumbani na Watunisia

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Yanga ilicheza na Club Africain uwanja wa kwa Mkapa na kutoa sare ya bilabila. Kwa anaefahamu mpira huu ulikuwa ushindi mkubwa kwa Yanga, hata Club Africain wenyewe wanalitambua hili.

Cha kushangaza wachambuzi uchwara na Makolo wanataka kuwaaminisha watanzania, wapenzi na wadau wa Yanga wote kuwa Yanga ni dhaifu, wachezaji hawafai, kocha hafai na uongozi haufai kwa yanga kupata sare ya 0-0 kama kwamba hawajui kwamba hata Al-Hilal na Club Africain ni timu kubwa sana Afrika na wanastahili kufungwa tu Yanga. Anaeamini kwenye upuuzi kama huu sio mwanamichezo bali ni mshabiki maandazi au anatafuta ahueni ya timu yake kwa Prof. Nabi na benchi lake la ufundi kufukuzwa na kuitafutia Yanga migogoro.

Kama yuko mwanayanga anaeamini kuwa kwavyovyote vile Yanga inastahili kuzifunga timu zote za nje ya nchi mshabiki kama huyo ni mjinga na mbumbumbu wa michezo anaejifanya ana uchungu mkubwa na Yanga kuliko Eng. Hersi au GSM anaemimina fedha zake.

Nijuavyo mimi Club Africain sasa hivi wana wasiwasi mkubwa kuzidi ule walionao Yanga, kwakuwa wanajua hata sare kwao haiwafai na wanajua Yanga ina wachezaji ambao wanaweza kupata goli kwenye uwanja wowote ule duniani.

Tuache ujinga na mihemko, hakuna ubishi kuwa Nabi hapendwi na timu zoote kwenye ligi. Ni mtu mpumbavu tu ambae atamfukuza kocha ambae anashinda timu zote kwenye ligi huko akijua kuwa ili upate nafasi ya kucheza mashindano makubwa lazima kwanza ufanye vizuri kwenye ligi yako kwanza.
 
Wazee wa mihogo mnajifariji[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Huyo atakuwa mnyama anawapiga madongo mihogo kwa lugha ya kejeli.... Stuka!
 
Ombeni msaada kwa Simba wanafanikiwa vipi mkakati wao wa kwa Mkapa atoki"NTU"mechi za kimataifa.

tafuteni wazee wenye hekma wakachutame kwa wazee wenzao kina Kaduguda na mzee Hassan Dalali wakaongee kiubwa.
 
Simba wanawezeshwa na TFF kwa kupangiwa ratiba nafuu kwenye ligi, kununua waamuzi na ulozi, baasi. Yanga kabla ya kucheza na Tunisia imetoka kucheza mechi ngumu na Simba, KMC na Geita back to back, wachezaji sio Play Stations
 
Mnalalamika wenyewe..Simba sisi tulalamike ili iweje..suala la muda tarehe tisa wala haiko mbali
 
Simba wanawezeshwa na TFF kwa kupangiwa ratiba nafuu kwenye ligi, kununua waamuzi na ulozi, baasi. Yanga kabla ya kucheza na Tunisia imetoka kucheza mechi ngumu na Simba, KMC na Geita back to back, wachezaji sio Play Stations
TFF wakiwaacha bila kucheza mechi ya mashindano malalamiko ya match fitness yanaanza. Mkipangwa mcheze mechi ili mpate match fitness bado lawama kwa TFF. kiufupi haya mashindano hatyuawezi iwe TFF watupe muda au wasitupe muda.

Sent from my Redmi Note 9 Pro using JamiiForums mobile app
 
Naona umeamua kuwafariji wala mihogo. Basi na wenyewe watajaa utafikiri africain huku walikuja kutafuta ushindi.

Ni hivi pla A ya timu yoyote inayoenda ugenini tena mechi ya kwanza ni kwenda kutoruhusu goli au sare ya namna yoyote ili gemu akaimalizie nyumbani.

Plan B, endapo atafungwa basi lisizidi goli moja ili kujipunguzia mlima wa kusawazisha nyumbani.

Plan C, kutafuta ushindi mwembamba ugenini walau wa bao moja bila.

Akifanikiwa moja kati ya hayo nafasi ya kumaliza kazi nyumbani ni kubwa kwa zaidi ya asilimia 90.

Kwenye mashindano ukishaona timu inaanza kuombea matokeo eti naombea nikatoe sare ujue ushaenda na maji kwa asilimia karibu zote dadekiko[emoji1787]. Wewe unaomba na mpinzani anaomba sasa hapo Mungu amsikilize nani[emoji2369]. Aliyejiandaa anashinda.

Wala mihogo mnaenda kuchagua mnasafirisha au mnazika huko huko
 
Simba wanawezeshwa na TFF kwa kupangiwa ratiba nafuu kwenye ligi, kununua waamuzi na ulozi, baasi. Yanga kabla ya kucheza na Tunisia imetoka kucheza mechi ngumu na Simba, KMC na Geita back to back, wachezaji sio Play Stations
Na al hilal ratiba ilikuwa ngum? Baada ya masaa 72 tim inaruhusiwa kucheza mchezo mwingine, yanga walicheza chini ya masaa hayoo?. Tuache kutafuta huruma, kiuhalisia timu yetu ni mbovu sana kimataifaa. Hap naanza kuamini yale mambo ya bahasha, pengine hizi mechi za ligi tunashinda kwa sababu ya tigopesa.
 
Niliacha kusoma pale ulpo sema al hilal ni kubwa kuliko yanga..kenge nyie mngelijua hilo toka mwanzo mngekua mmeshafudhu..mnawadharau watu wakishawagonga ndio mnajifanya underdog... nawakumbusha tu mlisema nyie ni timu kubwa kuliko wao..mmewazid pesa uwekezaji hadi quality ya wachezaji..na ukweli nyie ni pesambele fc
 
Haya mambo yote amesababisha zalan fc safari ilikuwa inaishia pale pale kwa mkapa.
 
Simba wanawezeshwa na TFF kwa kupangiwa ratiba nafuu kwenye ligi, kununua waamuzi na ulozi, baasi. Yanga kabla ya kucheza na Tunisia imetoka kucheza mechi ngumu na Simba, KMC na Geita back to back, wachezaji sio Play Stations
Na mtu alikufa kwake na taifa licha ya ratiba kubana nyie mlikuwa mnataka mpunzike week nzima sio wakati team ina viporo kibao manara kweli kawakamata masikia kila anachowaambia mnaamini tu.
 
Na mimi naamini TFF wanawauliza team kabla ya mechi kama watacheza au wacheze kwanza champions league na usikute waliulizwa wakasema tunataka kucheza ila leo lawama zote zinaenda kwa TFF ili wamtupie jumba bovu.
 
Walivyocheza na zalan hawakulalamika wameona mambo yamekuwa magumu wanaanza lawama.
 
Mbona threads as Yanga zimekua nyingi??!?
90% ya jamii sport kwa sasa ni Uto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…