ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Wamepita Marais wengi hapa Tanzania lakini ni Rais Samia mtoto wa Ardhi ya Kizimkazi ndio ameutendea Haki Mkoa wa Mbeya kulingana na hadhi yake.
Ilikuwa ni Kilio Cha mda mrefu Kwa Wana Mbeya ambacho hakuna aliyekisikia isipokuwa huyu mwanamke Rais Samia.
Umefanya mambo mengi sana ya kuacha alama Mkoani Mbeya,miongoni mwayo ni
1. Ujenzi wa Barabara ya Tanzam njia 4
2. Ujenzi wa Mradi mkubwa wa Maji mto Kiwira
3. Ujenzi wa Barabara za lami za Mitaa km 15
4. Ukamilishaji wa uwanja wa ndege wa Songwe na kuanza kujenzi wa cold room
5. Kuanza ujenzi wa uwanja wa Maonesho ya Kilimo 8/8 kuwa wa Kimataifa
6. Pamoja na miradi hiyo mikubwa ila kubwa kuliko ni hili la Stendi kuu ya Mkoa
My Take
Mungu azidi kukupa hekima na maisha marefu uje utujengee na uwanja mkubwa wa mpira maana watu wa Mbeya ni wanamichezo mahiri.
Tutasimulia Wajukuu alikuwepo Samia aliipa heshima Mbeya 🙏🙏
Pia soma Idadi ya miradi mikubwa inayotekelezwa na Rais Samia mkoani Mbeya
=====
MBEYA -Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mohamed Mchengerwa amesema ujenzi wa Stendi Kuu ya Mabasi na Soko katika jiji la Mbeya vitakwenda kuongeza thamani ya Jiji hilo kwani itaboresha upatikanaji wa huduma kwa wananchi.
Ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imetoa fedha zaidi ya Sh bilioni 30 kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu katika jiji la Mbeya.
Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa hafla ya utiaji saini Mikataba ya miradi ya ujenzi wa barabara, Kituo Kikuu cha Mabasi na Soko Kuu la Jiji hilo kupitia Mradi wa TACTIC iliyofanyika katika Viwanja vya Ndege vya zamani jijini Mbeya leo Julai 27, 2024.
Amesema ujenzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi eneo la “Old Airport” na Soko Kuu eneo la “Sokomatola” utagharimu Jumla ya Sh bilioni 30.12 na ni imani yetu sote pasina shaka kuwa miradi hii italeta mabadiliko chanya kwa wananchi wa Jiji la Mbeya na wageni mbalimbali ambao watanufaika huduma za usafiri na usafirishaji na ufanyaji wa biashara kwani nidhahiri kuwa thamani ya maeneo husika itapanda na hivyo kusababisha ongezeko la mapato kwenye Halmashauri.
Imeandaliwa na Mwandishi Wetu
View: https://youtu.be/m1oo21ZfKI0?si=2zRCHlTtVnd3wSDh