Asante sana JamiiForums, naingiza zaidi ya 50,000 kwa mwezi

Asante sana JamiiForums, naingiza zaidi ya 50,000 kwa mwezi

TEMBO WANGU

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2014
Posts
930
Reaction score
1,290
Wakuu habari zenu,

Naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa uongozi mzima wa JamiiForums maana nimekuwa nikifaidika kila mwezi kwa kupata kipato cha kununulia vocha mjini.

Niliweka post humu JF inayohusu kupeleka watu kwenye machimbo mbalimbali original ya bidhaa kwa bei ya jumla nikasema machimbo yoyote unayotaka wewe nitakupeleka.

Hii kazi ninafanya zaidi ya miezi sita, napeleka watu kwenye machimbo ya Kariakoo yanayouza vitu vya jumla kutoka kwa Wachina na wazawa hivyo uungwana ni kushukuru kwa platfom hii kwa kuwa napata elimu na pia napata kipato.

Asanteni sana JF. Kwa anayehitaji huduma hii niko free any time call 0757994417.

VIVA JF VIVA....
 
karibu Sana mkuu gharama ni 6000 nitakuonesha, nitakusaidia kununua,na pia nitakueleza changamoto za soko la kariakoo,maana biashara zingine zinautapeli Sana kwenye kununua.
Safi sana. Ukitaka upate mafanikio makubwa ni kuwa mwaminifu na usiwe na tamaa. Kuwa mkweli, bora ulale njaa kuliko kupata chakula leo kwa njia ya ulaghai. Hizi kanuni ni wabongo wengi hawapendi kuzifuata na ndiyo maana hatufanikiwi au kudumu kwenye kazi. Na zaidi usiwe na nyodo au ''kuvimbiwa'' mafanikio.
 
Wakati huohuo wewe machimbo yako ni MMU, kuna pesa huko?[emoji848][emoji848][emoji848]
Mimi MMU napata madini yatakayonisaidia kudumisha mahusiano yangu, acha kupenda material things sana wewe 🙋‍♂️

Afu usinikumbushe Kuna siku nilizunguka Kkoo kama pia nilipotea aisee sioni sehemu ya kupandia daladala kurudi home, kuulizia watu naogopa watanitapeli wakigundua ni wa kuja aargh😀😀
 
Ninyooshe tu maelezo, natafuta chimbo lenye simu original kwa bei poa,mahali ninapofanya kazi kuna wateja wengi sana,nimekuwa nikiwaagizia bidhaa tofauti na kupata faida kidogo inayonisaidia ku solve some issues,ila wateja wengi wanataka simu, saa, Tv, home theatres nk, ila huwa na take the highest risk kumtumia hela mtu nisiyemfahamu japo pia nashukuru kuwa sijawahi kutapeliwa kiujumla, ila kuna ile unaagiza kitu kwa lets say 100,000 halafu mtu anakuambia hii bidhaa inapatikana hata hapa kwa bei chini ya 80,000,na kweli ukimpa hela anakuletea, sasa hiyo huwa inapunguza imani kwa wale wateja waliokuwa wakiamini kuwa bidhaa zangu ni cheaper, nikaamini kuwa kuna machimbo mengine cheaper zaidi ya haya ninayoyategemea ya kwenye phone book.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom