Asante Yesu umetenda tena

Asante Yesu umetenda tena

verses fountain

Senior Member
Joined
Sep 30, 2018
Posts
155
Reaction score
194
Wakuu kwema? Wazima shkamooni.

Jina la Bwana Yesu Kristo lisifiwe milele na milele Amina.

Poleni na majukumu ya hapa na pale.

Niende kwenye Mada moja kwa moja..mimi ni mhitimu wa kozi ya afya kwa ngazi ya diploma nliyemaliza masomo yangu 2021 september.Baada ya kumaliza chuo na mapambano ya hapa na pale yakaanza kutafuta sehemu hata za kujitolea au kujishkiza(tunavyosemaga) ili kujiexpose na mazingira japo kwa kuanza nitoe tongotongo la shule kwa kufanya kazi kupata pia uzoefu zaidi kwa manufaa ya sasa na baadae kikazi na kitaaluma(usipofanya kazi hata shule uliyonayo kichwani inabebwa na upepo wa kisulisuli).Nilifanikiwa kufanya kazi kidogo kwenye zahanati moja hivi ila mazingira ya kazi yakawa hayaeleweki nikaona nitulize kichwa wakati nikitafuta namna ya kwenda mkoa mwingine ambapo kidogo kuna future ya kitu nlichosomea pamoja na exposure kubwa zaidi ya ishu za afya kwa ujumla nikilenga kujitolea kwenye ngazi kubwa zaidi ya taasisi ya afya.wakati muda unayoyoma na matangazo ya kazi pia yalikuwa yanatoka kwa upande wa mashirika kwa hyo ikitoka tu hivi wadau wakituma unafanya kuomba tu bila kujiuliza sana na mentality ya popote kambi ishaanza kutia mizizi kichwani kwa hyo likija unahakikisha ndani ya siku hiyo unatuma maombi huku ukisubiri majibu..

Siku moja nimekaa mchana baada ya kupeleka barua za kujitolea na maombi mengine sehemu mbalimbali mkoa wa ugenini nilipofikia,nikafungua email yangu nikakuta tangazo la kazi mkoa mwingine tena na nafasi ilikuwa moja nikajipa moyo kwani nikiomba nitapungukiwa nini kwanza sina cha kupoteza nkajisemea kwamba kama nlivyokuwa naomba kila inayokuja na hii pia ntaomba.nikatuma maombi yangu nikapotezea lakini Mungu alivyo wa maajabu siku sio nyingi nikaitwa kwa ajili ya Interview,nilijiandaa kweli sio haba na kwa vile ilikuwa ya kwanza sikua na idea nitaulizwa maswali ya aina gani kwa hyo kichwa kikazidi kupata moto zaidi ila baada ya kufanya utafiti binafsi wa interview kwa vyanzo tofauti JF(ibarikiwe JF kwa watu wenye +ve ideas & opinions msaada wenu mkubwa msiache kuandika thread zenye madini,huwezi kujua utasaidia /kumgusa nani) ikiwemo nikapata moyo inawezekana kufanya vizuri.Siku ikafika nikawah sehemu ya interview mapema,jina likaitwa la kwanza (japo nliandika wa mwisho kwa ushauri wa mwanaJF mmoja hahaa😀😀) nikanyanyuka na bahasha langu la khaki nikafika pale nikasalimia panel (watu sita)wakaniuliza maswali nikayajibu kwa uelewa nliokua nao bila kubabaika nikatoka nikiwa niko katikati nikishindwa kuelewa kwa namna walikuwa wananiinterivew kwa upendo ni ili kunifanya nisijiskie vibaya au ni baada ya kujibu maswali yao vizuri au?? Nilitoka nina maswali mengi kichwani ila nikiombea majibu yatoke vizuri maana mtaa ase hapana nlikua nimeshaanza kuuchoka kwa kweli.

Majibu yakatoka mchana baada ya siku kama 10 hivi nikafungua email harakaharaka nkiwa na mawazo mengi pia kwamba je nmelipata au ndo imenipita kushoto kama zingine?.Kuifungua nikakuta nimechaguliwa nilifurahi nikarukaruka nikaimba na kumshukuru Mungu kwa muujiza wake huo kwa sababu kuchaguliwa kwangu ninaamini sio kwa sababu ya kuwa smart kimuonekano, gpa,kujibu kwa usahihi maswali yao,chuo nilichosoma naweza nikasema neno moja tu kwamba ni kwa NEEMA ya Mungu nilichaguliwa ile nafasi pamoja na maombi ya watu ambao walikuwa wananiombea kabla na baada ya interview.Huu ni ushuhuda wangu kati ya shuhuda zangu ambazo nitazidi kuzileta huku kwa kadri Mungu atakavyonipa uzima zaidi.

Neno langu kwenu ni kwamba Tusikate tamaa, kila mtu ana wakati wake wa kupata kile ambacho Mungu amekuandalia tangu mwanzo.Amua kuweka Imani kwake usiwe na hofu kwa sababu ya maneno ya watu maana kuna mmoja aliniuliza vipi lakini una watu unawafahamu huko? Nilimjibu hata sina ninayemfahamu kule.nikajua ana wasiwasi kwamba bila kuwa na mtu nitakosa ile nafasi ila Mungu wa majaabu asiyelala wala kusinzia akajibu maombi yangu.

Itoshe kusema,Abarikiwe Mungu wa Mbingu na Nchi kwa yote na Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi nyote. AMINA
 
Ndefu sana sijasoma yote but naona itakuwa good news tu.

Hongera sana mkuu.

Ila kuna jinsia yetu hii ya Karucee. Ukikosea kuchagua tu imekula kwako.

Sasa ukute mtoa mada ni jinsia yangu nitajuta kutomaliza kusoma.😁😁😁
 
😁😁 shukran sana..ukiandika itaendelea hawarudi kusomaaa.. sijakuelewa mkuu jinsia ya karucee unamaanisha nini?
 
Ndefu sana sijasoma yote but naona itakuwa good news tu.

Hongera sana mkuu.

Ila kuna jinsia yetu hii ya Karucee. Ukikosea kuchagua tu imekula kwako.

Sasa ukute mtoa mada ni jinsia yangu nitajuta kutomaliza kusoma.😁😁😁
Kafanyiwa interview, Yesu Kampa majibu, sasa kaja kushukuru
 
Hongera Chief.Lkn jua una dhima kubwa katika hiyo kada ya afya.Tenda haki
shukran mkuu...ninatambua hilo mkuu na ninaamini nitaitendea haki taaluma yangu na nafasi niliyopewa ni dhamana kubwa hivyo nisipotimiza ninachopaswa natambua wazi nitashushwa na kunyenyekezwa kwa kadri Mungu atakavyoona ni sawa.
 
Hongera kiongozi kumrudishiabMungu shukrani. Mwenyewe leo kimenitokea kitu ambacho nisipomshukuru Mungu nitakuwa nimepungukiwa kikubwa.

Leo imetokea ajali wakati nikitokea Kibaha kuja Dar mchana wa leo. Daladala nililokuwa nimepanda lilijariribu kuikwepa gari iliyokuwa inakatisha barabara bila kuchukua tahadhari. Nikiwa sina hili wala lile nkifatilia Urusi na Ukraine ghafla nkasikia makelele ya kina mama na ghafla nkaona gari inayumba kushoto na kulia. Ndani ya muda mfupi nikajiona niko chini gari ishalalia upande na kila mtu anatafuta njia ya kutokea. Mimi nikabahatika kutokea dirishani nikiwa salama usalimini nikiwa tu na mchubuko mkono wangu wa kushoto. Kuna watu wamevunjika mikono kama wawili na dogo mmoja kachubuka uso. Kizuri hakukukuwa na kifo.

Ndugu zangu mimi namshukuru Mungu kwa kunitoa mzima wa afya nkiwa natembea mwenyewe. Mungu ni wa ajabu kiukweli. Wake waliobahatiks kupita barabara hiyo mchana huu maeneo ya Gogoni mtakuwa mashahidi wa ajali hiyo. Tizidi kumtanguliza Mungu.
 
Ndefu sana sijasoma yote but naona itakuwa good news tu.

Hongera sana mkuu.

Ila kuna jinsia yetu hii ya Karucee. Ukikosea kuchagua tu imekula kwako.

Sasa ukute mtoa mada ni jinsia yangu nitajuta kutomaliza kusoma.[emoji16][emoji16][emoji16]
Mbona unatutisha mkuu tulio kwenye searching spree
 
Hongera kiongozi kumrudishiabMungu shukrani. Mwenyewe leo kimenitokea kitu ambacho nisipomshukuru Mungu nitakuwa nimepungukiwa kikubwa.

Leo imetokea ajali wakati nikitokea Kibaha kuja Dar mchana wa leo. Daladala nililokuwa nimepanda lilijariribu kuikwepa gari iliyokuwa inakatisha barabara bila kuchukua tahadhari. Nikiwa sina hili wala lile nkifatilia Urusi na Ukraine ghafla nkasikia makelele ya kina mama na ghafla nkaona gari inayumba kushoto na kulia. Ndani ya muda mfupi nikajiona niko chini gari ishalalia upande na kila mtu anatafuta njia ya kutokea. Mimi nikabahatika kutokea dirishani nikiwa salama usalimini nikiwa tu na mchubuko mkono wangu wa kushoto. Kuna watu wamevunjika mikono kama wawili na dogo mmoja kachubuka uso. Kizuri hakukukuwa na kifo.

Ndugu zangu mimi namshukuru Mungu kwa kunitoa mzima wa afya nkiwa natembea mwenyewe. Mungu ni wa ajabu kiukweli. Wake waliobahatiks kupita barabara hiyo mchana huu maeneo ya Gogoni mtakuwa mashahidi wa ajali hiyo. Tizidi kumtanguliza Mungu.
mkuu poleni sana...Inafika muda inabidi ushuhudie kwa faida ya wote..wanaoamini na wasioamini Uwepo wa Mungu na nguvu zake.ninaamini kuna ambao wameguswa zaidi wataguswa na ushuhuda wako.kila sekunde ya uhai ni baraka kubwa sana ambayo haitakiwi kuchukuliwa kiurahisi.
 
Back
Top Bottom