Asanteni kwa kusikia kilio chetu cha foleni Mwenge asubuhi. Jioni pia ruhusuni magari kwa usawa pande zote

Asanteni kwa kusikia kilio chetu cha foleni Mwenge asubuhi. Jioni pia ruhusuni magari kwa usawa pande zote

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Ndugu zangu kwema?

Kama kuna jambo zuri limefanyika sio mbaya tukipongeza. Barabara ya Mwenge kama mwezi hivi umepita kulikuwa na tabia ya magari yanayotoka Tegeta kupendelewa zaidi kwa kuruhusiwa kupita barabara zote.

Soma:
Adha ya foleni katika makutano ya barabara ya Mwenge

Pamoja na kutatua tatizo hilo bado shida kubwa na utaratibu mbovu wa kuruhusu magari ipo eneo hilo muda wa jioni. Matrafki wamekuwa wakiruhusu magari ya kutoka mjini kwenda Mbezi Beach kwa upendeleo mkubwa na kuacha pande nyingine kwa muda mrefu.

Hivyo tunaomba mamlaka husika ziweke taratibu nzuri za kuruhusu magari kwa usawa maana Watanzania wote wana haki sawa ikiwemo kuwahi nyumbani jioni.

Nawasilisha.
 
Gari zinazotoka tegeta kwa asbh ni nyingi san lazima neptism iwepo tu, kwa jion gari zinazotoka Morocco ni nyingi sana lazima upendeleo uwepo tu.
 
Back
Top Bottom