ibra87
R I P
- Jul 22, 2015
- 5,614
- 5,351
Wasalaam wana MMU!
Ninayaandika haya nikiwa ni mwenye furaha iliyopitiliza.Furaha Ambayo imenifanya nije hapa kuja kuwashukuru wana mmu walioamua kuacha kazi zao na kuja kuungana na mimi kunisapoti katika siku yangu ya kuzaliwa.
Sikutegemea wala kuamini kile ambacho mlikifanya jana kwa ajili yangu.Hakuwa mama, wala baba waliokiamini kile mlichofanya.Hawakuwa dada zangu au kaka zangu waliwaza kwamba kitafanyika kitu kama kile. Wote tulibaki kushangaa na kutokuamini kinachotokea.
Mlijitoa kwa hali na mali mkashiriki nami mpaka usiku wa manane bila kuchoka. Mlinipa zawadi ambazo zimenifanya niamini na kutambua kuwa japo kuna wengi ambao hawanipendi lakini vile vile nikajua wapo wengi tena sana wanaonipenda na kunipenda kupika kiasi. Wengine hamkuwahi kuwa nje ya makwenu mpaka usiku wa manane, lakini kwa ajili ya ibra87 mlifanya hivyo.Hamkuwahi kuvuka bahari lakini kwa ajili ya ibrah87 mkafanya hivyo...
Nashindwa jinsi ya kuwashukuru lakini tambueni nimehemwa kwa kile ambacho mlinifanyia siku ya jana.Ahsante wewe dada ambae ulijitolea gari yako kwa ajili ya usafiri wa kututoa nyumbani na kuturudisha nyumbani pia kuwapeleka baadhi ya wana mmu wenzetu majumbani kwao.
Umenionyesha moyo wa upendo na kunikumbusha vitu vingi sana ambavyo nimepitia.Nilishindwa kujizuia nikalia kwa furaha na uchungu lakini ulinifuta machozi na kuniambia usilizwe na yaliyopita.
Mama na baba pamoja na ndugu zangu walipigwa na butwaa baada ya kuona ulipokuwa unanifuta machozi kwa upendo wa hali ya juu.Wakazani labda ni mkwe na shemeji yao lakini hawakuujua ukweli kuwa wewe ni rafiki tu.Nilitamani nikwambie kitu ama nikutaje jina hapa lakini kwa maneno yako uliyoniambia ya kwamba wakati bado nayaheshimu sana.
Kwa kumalizia kusema nasema ahsanteni sana kwa kunijali, kunithamini na kunipenda.Tuendelea kuwa hivi mpaka pale mungu atakapo tuchukua kwa niaba ya familia yangu napenda kuwashukuru na kuwafikishia shukurani hii.
Wenu
ibrahim h masimba
muwe na siku njema