LGE2024 Asanteni Watanzania kwa kuendelea kuiamini CCM

LGE2024 Asanteni Watanzania kwa kuendelea kuiamini CCM

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Chama cha Mapinduzi kinatoa shukurani za dhati kwa wanachama wake, wakereketwa,wafuasi na watanzania wote kwa ujumla wake kwa kukipigia kura nyingi za ndio na hivyo kukiwezesha kushinda kwa kishindo kikuu kilicho itetemesha Dunia nzima.

Chama cha Mapinduzi kinaahidi kuendelea na kazi ya kuwatumikia watanzania na kuwaletea maendeleo na ustawi wa Maisha yao ya mwananchi mmoja mmoja na Taifa zima kwa ujumla wake.

Viongozi waliochaguliwa wamejipanga kutoa na kuwatumikia watanzania kwa utumishi uliotukuka na wenye kujali maisha ya watanzania pasipo ubaguzi wa aina yoyote ile na kwa misingi ya Aina yoyote ile Zaidi ya utanzania .Watu wote watahudumiwa kwa haki na kwa unyenyekevu wa hali ya juu sana.

Uchaguzi umekwisha na kilichobakia ni kuendelea na kazi ya kuwatumikia watanzania wote.Tuungane kwa pamoja kulijenga Taifa letu.tulinde kwa wivu Mkubwa sana tunu yetu ya Amani na utulivu wa Taifa letu.Ni katika amani na utulivu ambapo kila mmoja wetu anaweza kutimiza ndoto zake na kujiletea maendeleo Binafsi
Screenshot_20241129-175138_1.jpg


Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Back
Top Bottom