Akizungumza leo Aprili 27 katika mkutano wa asasi za kiraia 14 zilizotoa msimamo kuhusu Tume ya Jaji Othman Chande, Mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu chaa Dr es Salaam, Dk Azaveli Lwaitama amesema hawakubaliani na pendekezo la tume hiyo kutaka iundwe tume nyingine ya kuchunguza jinai, badala yake wametaka kuundwa kwa tume huru ya kutafuta ukweli, uwajibikaji, na maridhiano ya kitaifa itakayoongozwa na watu huru.
Pia wametaka Serikali ilipe fidia kwa wahanga wote wa matukio ya Oktoba 2025, waliofariki na waliojeruhiwa, kwa kuzingatia sheria na mikataba ya kimataifa.
“Mchakato wa Katiba Mpya uanze baada ya kupata mwafaka wa kitaifa na uwajibikaji kwa yaliyotokea ili kuzuia kurejea kwa matukio kama hayo. Wafungwa wote wa kisiasa wanaoendelea kushikiliwa, akiwemo mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu, waachiwe mara moja bila masharti.