ASEC Mimosas kulipa fadhila kwa Wydad Casablanca

ASEC Mimosas kulipa fadhila kwa Wydad Casablanca

TUKANA UONE

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2018
Posts
2,345
Reaction score
6,970
Hivyo ndivyo ninavyoweza kusema kwasababu kama tunakumbuka fainali za mataifa ya Afrika yametamatika hivi karibuni na Bingwa kuwa muandaaji wa michuano husika yaani Cotè d'ivoire.

Kama mtakumbuka;

Baada ya Cotè d'ivoire walipenya kwenye tundu la sindano na hii ni baada kupita kama Best looser kwenye kundi lake, hii ni baada ya timu ya Morocco kuichapa Zambia kwa bao moja kwa bila, hivyo basi kuanzia hapo Cotè d'ivoire ikampa sifa zote Morocco na kusema wao ndiyo wamefanya wakasonga mbele.

Sifa hizo hazikuishia mdomoni tu,bali wananchi wa Cotè d'ivoire walibeba bendera za Morocco na kuzipeperusha huku wakiimba na kuwapatia sifa kemkem.

Hivyo basi, naona kabisa timu ya ASEC Mimosas kwakuwa wao wameshapenya kwenye Robo Fainali, nadhani wanaweza kuwaachia mwanaya hawa Wamorocco ili nao waweze kupenya kuingia Robo Fainali kwa kuwafunga. Kiukweli sioni kama ASEC Mimosas watawakazia hao Wydad kwasababu ya nilichokieleza hapo juu.

Jambo pekee ambalo Simba anapaswa kufanya kwa Mkapa ni kushinda na wala si vinginevyo!

Simba wakiingia kwa dharau kwa kuwachukulia poa Jwaneng Galaxy wanaweza wasiamini macho yao kwasababu hao Galaxy nao hesabu zao zipo kwa Simba. Pia Simba wasiingie kwa kupania sana maana pia wanaweza wasifanye vizuri.

Nikiwa kama Shabiki wa kutupa wa Young Africans nawatakia ushindi Simba nikitambua ya kwamba,Bila Simba imara hakuna Yanga imara, na bila Yanga imara hakuna Simba imara.

Naamini Makolo mtafanya vizuri kama sisi ndugu zenu Utopolo tulivyofanya vizuri.
 
Back
Top Bottom