Aseno Wenger out!

last king of uscoch

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2015
Posts
2,728
Reaction score
3,980
Ndugu wana jamii forum,ndugu wana ligi kuu ya uingereza(EPL) na wapenzi wa burudani wote habarini za mihangaiko ya hapa na pale ya maisha.
Nipende kuweka wazi tu kuwa Mimi si mshabiki wa arsenal,ila ni mshabiki wa Chelsea na mpenzi wa ligi kuu ya uingereza(EPL),Kinachonisumbia na kunikereketa ni kuiona arsanal kila Mara ikifanikiwa kuingia katika nne bora ya ligi lakini mwisho wa siku wa nakuja kuboronga mwishoni na kuitia aibu EPL yote,ni kwanini wasibadili mbinu? Mikakati n.k?,Hivi huyo Wenger ananini na arsenal? Kwanini asiondoke? Embu naomba nipewe angalau hata mawili matatu juu ya huyu kiumbe na arsenal kuna nini nyuma ya pazia? Naomba majibu hata kwa tetesi tu kama majibu yalivyo kwa barshyte na mkemia embu nipe na ya huyu kocha,
 
Yanga kamkimbia Simba.
Huyu simba zamani alikuwa punda, yanga kachoka kuumizwa πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Wenger ndiye anayetafuta hela kuendesha arsenal. Wengine tunashangilia sana bila kuchangia
 
Issue za kwingine zinakuhusu nini? Makosa na mapungufu ya mpinzani wako mchezoni ndiyo mafanikio yako. Acha unaa wewe
 
Nimekuja resi nkajua keshatemeshwa blah blah blah
 
Mkono wa mamlaka tumbuaji haufiki kwa the gunners?
 
Mimi ni mshabiki wa Arsenal nasema:

Arsenal Wenger OUT.

Amechoka yule mzee...sijui amekula maharage ya wapi?
 
Msichokijua ni kwamba pamoja na Wenger kuwa kocha lakini pia ni mmiliki wa timu! Ana hisa za kutosha tu pale Arsenal! Wakikaa jopo LA wamiliki na yeye yumo!
Lakini pia mbinu za Wenger zimeitajirisha sana Arsenal! Kwa hiyo bodi ya Arsenal haiwezi kumfukuza Wenger labda aamue mwenyewe kupumzika kama alivyofanya Furgurson! Vinginevyo mtasubiri sana jamaa kutumbuliwa!
 
Wenger hana hisa arsenal kama watu wanavyoamini... anayemkumbatia wenger ni Stan kroenke mmarekani mwenye hisa nyingi za club na ndiye anayeonekana ana nguvu zaidi. Lakini baadhi viongozi wengine wa club hawamtaki na wanaamini Wenger uwezo wake wa kuiongoza arsenal umeeishia pale. Na kuna taarifa za chinichini zilizotoka jana Chief executive wa arsenal bwana Ivan Gazidis ametishia kujiuzulu kama Wenger akiendelea kuwa kocha wa arsenal. Ni mmoja wa watu ambao Wenger ameingia nao bifu kubwa ndani ya club, kwasababu jamaa alimchana kwa kumwambia uwezo wake umeisha na anawagawa mashabiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…