Asgard Security Company Limited: Ufafanuzi kuhusu madai ya kutolipa wafanyakazi mshahara

Asgard Security Company Limited: Ufafanuzi kuhusu madai ya kutolipa wafanyakazi mshahara

Status
Not open for further replies.

UlinziImara

New Member
Joined
Feb 18, 2025
Posts
1
Reaction score
0
UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA ILIYOCHAPISHWA IKITUHUMU KAMPUNI YA ASGARD SECURITY COMPANY LIMITED KUTOLIPA WAFANYAKAZI WAKE MISHAHARA

Mnamo tarehe 17 Februari 2025, kwenye Mtandao wa Jamii Forums na kurasa zake katika mitandao mingine ya kijamii ilichapishwa habari iliyotoka kwa mwananchi inayodai kampuni ya Asgard Security Company Limited kulalamikiwa na baadhi ya wafanyakazi wake kwa kutolipa mishahara na kwamba hutishiwa kufukuzwa kazi pale wanapodai stahiki zao.

Zaidi soma >> DOKEZO - Walinzi Kampuni ya Asgard Security hatujalipwa mishahara kwa miezi miwili, tukifuatilia uongozi unatishia kutufuta kazi

Tunapenda kuomba radhi na kukanusha taarifa hiyo kwakuwa haina ukweli wowote. Tayari uongozi wa kampuni umewasiliana na JamiiForums kukanusha madai hayo.

Aidha kampuni inapenda kueleza kwamba inathamini huduma zinazotolewa na wafanyakazi wake na kwamba inazingatia haki na stahiki zote za wafanyakazi ambazo zipo kwa mujibu wa sheria. Wafanyakazi wote wa kampuni wapo kwenye majukumu yao ya kikazi na endapo kuna malalamiko yoyote yanashughulikiwa kikamilifu kwa mujibu wa utaratibu wa kiofisi.

Kampuni inapenda kutoa rai kwa wadau wa huduma zake kwa ujumla kutokuwa na shaka juu ya uadilifu wa uongozi wa kampuni husika na weledi wa utendaji kazi kwakuwa inazingatia misingi ya haki na kuthamini uaminifu ambao inapata kutoka kwa wadau wake na kuahidi kwamba itaendelea kujiboresha ili kuhakikisha wateja wanapata huduma yenye viwango vya juu kabisa katika kuhakikisha usalama wao na wa mali zao.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom