Asha Baraka: "Sitaki Ali Choki afie kwangu''

Asha Baraka: "Sitaki Ali Choki afie kwangu''

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598
ASHA BARAKA CHOKI.jpg
Baada ya msanii wa mziki wa Dance Ali Choki kupiga stori na eNEWZ wiki chache zilizopita na kusema mwaka 2018 atafanya kazi zake mwenyewe kama Mama Asha Baraka ataendelea kulala, kiongozi huyo wa Twanga Pepeta amemjibu Choki.

Mama Asha Baraka baada ya kusikia kauli hiyo amesema anamshangaa sana Ali Choki kusema maneno hayo kwani tangu mwaka jana alishamruhusu akafanye kitu anachotaka hata kama ikiwa ni pamoja na kazi zake binafsi.

''Namshangaa sana Ali Choki mimi nishampa ruhusa afanye kazi nyingine yoyote bila kujali mkataba wetu unasemaje hivyo yeye aendelee na mambo yake wala asinifikirie'' amesema.

Asha Baraka pia amesema kuwa hataki Ali Choki afie Twanga Pepeta hivyo kama ana uwezo arudi akaifufue Extra Band kwani alimpa uongozi ndani ya Twanga Pepeta akashindwa kuiongoza.

Ali Choki tayari ameshaonekana akiingia studio na msanii Beka Flavour kuandaa kazi zake binafsi hivyo huenda akawa tayari ameshajiandaa na maisha bila ya Twanga Pepeta.


EATV.
 
sidhani kama unamjua Ally Choki, amechoka vibaya. Last time nimemuona yupo na King Kikii bar fulani nikawa nabisha sio yeye hadi alivyojitambulisha na kuimba kidogo.
na pia asha kwani amesema kufa ipi kimziki ama kifo kile kingine maana nadhani hii ni tungo tata
 
Unachoongea hukijui, nafikiri unamfanaisha Choki na Msafiri Diof ambaye ndo kanenepa sana. Kwa Choki umebugi
hapana namfahamu choki toka utotoni mwangu wacha kunilazimisha kukubali unachoniambia wakati nimemuona mwenyewe na kuna mtu alimwagia pombe lwiza mbutu akalalama sana n way yeye ni mwanadamu kila mwanadamu ana ups and downs................ kama kachoka sawa tu hata mie na wewe tunaweza kuchoka pia kwani yeye nani mpaka asichoke? mpe pole ukimuona na leo
 
Back
Top Bottom