Asha Baraka: "Sitaki Ali Choki afie kwangu''


asha baraka yuko sawa kabisa....tatizo elimu hakuna choki..
 

Ina maana hakurithishwa chochote..?
 
Huyu Choki alitembelea nyota ya Banza Stone na huyu Asha Baraka hana lolote na mikorogo yake, wote zilipendwa.
Ila hii habari ya Choki alitembelea nyota ya Banza hainaga mashiko kabisaaaa.....ni mawazo ya watu wanaokosa kufanya ulinganifu sahihi.

Banza alianza 1999 na Choki 2000 katika Twanga, ila niambieni nani ametunga hits nyingi ndani na nje ya Twanga Pepeta? Album ya kwanza ya Twanga Banza alitunga wimbo wa kumekucha haukuhit sana, albamu ya pili kabla hajaondoka alitunga Aungurumapo Simba kisha akaondoka kwenda TOT. Huko TOT nakiri alitunga nyimbo kadhaa nzuri mfano Mtaji wa Masikini, Aungurumapo Simba 2 na Elimu ya Mjinga. Aliporudi Twanga 2004 'akatunga' MTU PESA (ukumbuke mashairi ya Mtu Pesa yalikuwa ni yale maandishi ya vile vibao vya ukutani).Mbali ya hapo alijaribu kuwa ba bendi ya BAMBINO ( Banza na Mbizo Juma) lakini haikufanya vyema na hapo wakatoa collabo Choki, Muumin Mwinyijuma na Banza kile walichokiita Mafahari watatu kisha kikafa. Hapo ilikuwa sasa ni 2004 na Banza akarudi Twanga na wimbo wa Mtu Pesa.

Ali Choki yeye alipoingia Twanga akatunga wimbo wa Jirani pamoja na Tabu za Maisha kwenye albamu ya Jirani. Albamu iliyofuata ilikuwa ni Fainali Uzeeni akatunga wimbo wa Umbea hauna Posho na Busu la 2001. Albamu iliyofuata ilikuwa Chuki binafsi akatoa wimbo wa Chuki Binafsi na Engineer Saudia. Ikafuata album ya Ukubwa jiwe hakuwapo, album ya Mtu Pesa hakuwapo na Album ya Safari 2005 pia hakuwapo. In between hapo alikuwa na Extra Bongo awamu ya kwanza ikitamba kwa nyimbo kama Double Double, Extra bongo x3 na Regina, kisha akaenda Mchinga kwenye Ile Generation 8 baadaye TOT kwenye TOT Respect kabla ya kurudi Twanga mwaka 2006 na kutoa wimbo wa Mwana Dar es Salaam uliopata tuzo ya wimbo bora wa Kili Awards 2007.

Sasa ukiangalia kwa ujumla utaona Ali Choki alifanya Vizuri kuliko Banza maana usisahau Choki alipoifufua Extra Bongo ya pili alimuajiri Banza kama muimbaji.

Kiukweli kwa mtazamo wangu Ali Choki amefanya vizuri zaidi ya Banza utofautini kwa kuwa Banza alianza kabla ya Choki so akajijengea fans base lakini la pili ni haiba . Ali Choki haiba yake ndiyo ilimuangusha maana hakuwa mchangamfu kuliko Banzastone hivyo watu wakaona kama anajisikia na kumpenda Banza. Lakini kimuziki nina imani Ali Choki alikuwa mzuri zaidi ya Banza kwa muono wangu.
 
dah mkuu ama kwa hakika wewe ni mfuatiliaji nguli wa muziki wa dansi. ni kweli kabisa wote wamehit ila choki ana nyimbo nyingi zaidi zilizohit. kilichomsaidia banza pia ni ile hali yake ya uhuniuhuni usiombe wakae pamoja hapa banza pale msafiri diouf pale hadija mnoga kimobitel halafu umuongeze semsekwa utafurahi. ila alichoki alikuwa mtu wa kujiheshimu sana. tatizo tu ukimwi umewachukua wengi katika kizazi chao mpaka makuwadi wao kina Steve nyerere nae yupo kwenye orodha.
 
kwani mwanae? mshahara si alikuwa anapata " kakalia politic...sasa hali mbaya..

Ha ha ha.. Halafu dizaini hiyo kunakuwaga na ndugu zake mwanamke ambao wanakuwa wanachukia sana kitendo cha kumuona mwanaume akila mali za ndugu yao kwa kujifanya ana mahaba.. So ikitokea tu amededi, ndugu wanakuja kwa speed ya ajabu na kukutoa nduki..
 
Hakurithi hizo Mali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…