PostGE2025 Asha-Rose Migiro: CHADEMA hawakukatazwa wala hawakunyimwa fursa ya kushiriki Uchaguzi

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, akifanya mahojiano na Salim Kikeke, Crown Media


Your browser is not able to display this video.

​
Salim Kikeke: "Tukiangalia kwenye siku ya ya uchaguzi, baadhi ya vyama vya siasa vinasema kwamba uchaguzi haukuwa huru, haukuwa wa haki na pengine baadhi ya kundi la wananchi walishindwa kupiga kura kutekeleza haki yake ya kikatiba. Na ikawa ni kama moja ya vishawishi vya vurugu za Oktoba 29.

Asha-Rose Migiro: "Siasa yetu ni siasa ya vyama vingi na tunavyo vyama vingi vyenye usajili wa kudumu. Kama nilivyosema hapo awali, vyama hivi vyote, kikiwemo chama chetu, Chama cha Mapinduzi, tulishiriki katika mchakato wa kampeni. Vyama vilishiriki takriban 18. Sasa ni vyama gani vya siasa ambavyo vilikatazwa au vilinyimwa fursa ya kushiriki? Ni vyama gani?

Salim Kikeke: "Chama kikuu cha upinzani, Chadema, kilikosa nafasi, kilisema kwamba kilikuja na msimamo wa 'no reforms, no elections'. Hakuna mabadiliko, hakuna uchaguzi. Hauoni kwamba wafuasi wa chama cha Chadema walikosa haki yao ya msingi ya kupiga kura?

Asha-Rose Migiro:"Kwanza wenzetu wa Chadema hawakukatazwa wala hawakunyimwa fursa ya kushiriki. Na utakumbuka swala la wao kutoshiriki lilianza miezi michache tu kabla, 'hatutashiriki kama hakuna mabadiliko'. Lakini mabadiliko yalikuwepo na hiyo inajulikana wazi kabisa. Kabla ya uchaguzi huu, tume ya uchaguzi kupitia sheria iliyoundwa wakati ule ilifanyiwa marekebisho makubwa, muhimu.
 
Wabunge wameingia Bungeni bila kujua idadi ya kura zao.
 
Nilitaka k Nilitaka kumaliza MB zangu kizembe sana
 
Some more "Tanzanian Exceptionalism" bullshit.
 
Huyo inasemekana ni msomi halafu anaongea huo utumbo. Wale ambao hawajasoma wana hali gani?
 
Shida ya nchi hii inalazimisha kila mtanzania awe chawa..ukisikiliza majibu ya viongozi haramu wakijibu maswali ya msingi utaelewa tu kua taifa limebakwa
 
Faki zati bi+ch!

CHADEMA walifungiwa kufanya shughuli za kisiasa tangu 10 June 2025 mpaka walipofunguliwa na Mahakama ya Rufaa 15 April 2026!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…