Ashakum si matusi-taswa mmechanganyikiwa

Ashakum si matusi-taswa mmechanganyikiwa

TUMY

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2009
Posts
705
Reaction score
93
Muharami aibuka mwanamichezo bora Novemba
Napenda tena kuwaomba radhi kusema Taswa mmechanganyikiwa ila sifuti kauli yangu unless otherwise mtani prove wrong,Nimesoma kwa masikitiko habari kwamba golikipa Muharani amechaguliwa kuwa mwanamichezo bora wa mwezi Novemba,ameshinda kwa kipi hasa alichokifanya cha kishujaa sababu mliyoitoa eti yeye ndiye aliye isaidia klabu ya Ferroviario ya Msumbiji kuchua ubingwa haina uzito hata kidogo msitake kututania nyie, nani asiye mjua Muharani amekwenda na Taifa Stars Challenge huko Kenya hakuna chochote cha maana alichokifanya tumemuona kwenye mechi na Rwanda amefungwa magoli ya kizembe kabisa, anadaka utafikiri anadaka panzi, nafikiri mlikosa mtu wa kumpa hiyo zawadi mkaona isiende bure, hawa waandishi wa habari wa michezo wa Taswa sidhani kama mnatumia vigezo sahihi kuchagua mshindi ama na nyie mnaleta politics sasa, Muharami si kipa bora kiasi cha kusema ni yeye aliisaidia timu yake kuwa bingwa huo ni uwongo mtupu, halafu pili si kweli kwamba kufika kwa Muharami katika ile kabla ndio wao wakachukua ubingwa kamawalikuwa hawajawahi kuchukua na alipoffika yeye ndo wakachukua ingekuwa kigodo inaingia akilini ila hakuna sasa mmempa kwa kuwa Maximo amemuita,Muharami hana kiwango chochote acheni kuzuzuka kwa kuwa anacheza msumbiji.Mmekuwa mkikurupuka tu.Lets be realistic.
 
OK Toa maoni nani alistahili hiyo tuzo?
 
Back
Top Bottom