Ashauri Katiba ya Zanzibar iandikwe upya

Ashauri Katiba ya Zanzibar iandikwe upya

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,801


HABARI
[h=1]Na Mussa Juma, Arusha [/h]
Posted Alhamisi,Februari7 2013 saa 20:24 PM



KWA UFUPI
Mbunge wa Jimbo la Wawi (CUF), Hamad Rashid, alitoa wito huo jana mjini hapa, wakati akizungumza kuhusiana na mchakato wa katiba unaoendelea sasa na pia uwapo wa Katiba ya


SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar, imetakiwa kuiga Serikali ya Muungano, kwa kuanza sasa mchakato wa kuiandika upya Katiba ya Zanzibar ambayo inakabiliwa na upungufu kadhaa, ukiwamo wa kutowekwa vizuri muundo wa Serikali ya Umoja wa kitaifa.


Mbunge wa Jimbo la Wawi (CUF), Hamad Rashid, alitoa wito huo jana mjini hapa, wakati akizungumza kuhusiana na mchakato wa katiba unaoendelea sasa na pia uwapo wa Katiba ya Zanzibar. Alisema mchakato wa kubarekebisha ama kuandikwa upya Katiba ya Zanzibar ni wa lazima kwa sasa ili kuepusha michanganyiko kwa watendaji na kwamba marekebisho hayo yatakwenda sambamba na ya bara.


“Ni wakati mwafaka sasa Serikali ya Zanzibar kuona umuhimu wa kuanza sasa mchakato wa kuibadilisha Katiba ya Zanzibar kwani pia inaweza kuguswa sana na mabadiliko ya Katiba ya Muungano”, alisema Rashid.


Alisema miongoni mwa mapungufu yaliyopo sasa kwenye Katiba ya Zanzibar ni Tume ya uchaguzi kuwa ndio yenye uamuzi wa mwisho baada ya kutangaza matokeo,mfumo wa Serikali ya umoja wa kitaifa kitowekwa vizuri na pia hakuna mpangilio mzuri wa utekelezaji wa majukumu ya Serikali na sera.



“Nadhani kuna kila sababu ya Wazanzibar kukaa na kuipitia Katiba yao na hili ni jambo ambalo lipo wazi katika mazingira ya sasa ili kuwe na katiba bora”alisema Rashid.
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 imefanyiwa marekebisho kadhaa kwa sasa, ikiwamo kuongeza Serikali ya Umoja ya kitaifa na masuala ya Tume huru ya uchaguzi.



Hata hivyo, katiba hiyo, huenda ikaathiriwa na Katiba Mpya ya Muungano, ambayo ipo katika mchakato wa kuandikwa upya na mwezi Novemba rasimu ya katiba hiyo, inatarajiwa kufikishwa bungeni na baadaye itapelekwa katika Baraza la Katiba na imepangwa kukamilika Aprili mwakani


 
Wana katiba ya Amani Karume ya mwaka juzi, ile iliyo ondoa kuwa Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, badala yake kaandika Zanzibar ni Inchi. sidhani kuwa kuna yeyote alieshirikishwa katika kuandikwa.
 
Nadhani Hamad Rashid ameanza kuona ukweli na kurudi katika mstari!

Katiba ya Zanzibar haina budi kuandikwa baada ya kukamilika kwa katiba ya Tanzania ili iweze kujumuisha mambo ya muungano vinginevyo kunaweza kuwa na migongano!

Hongera Hamad kwa kutambua kuwa Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!
 
Back
Top Bottom