ASIEVISHWA KILEMBA.

ASIEVISHWA KILEMBA.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
ASIEVISHWA KILEMBA.


1.Hivi kwanza mnajua,napiga kimya Kwanini
Kipo msichotambua,niseme wazi ya nini
Hasara kumuumbua,asijevaa kipini
Asievishwa kilemba,hawezi kufunga domo.


2.Domo atalibenua,ahisipo ya rohoni
Yote atayocheua,ni yake ya utotoni
Ahisie anajua,mwacheni awe ndotoni
Asievishwa kilemba,hawezi kufunga domo.


3.Kile achojihisia,hakimkai kooni
Mbona atakiachia,kama watu awaoni
Kote atahadithia,afikapo kituoni
Asievishwa kilemba,hawezi kufunga domo.


4.Mwenye mguu wa bia,kujisitiri machoni
Hawezi kufikiria,iyonwapo yake mboni
Mbele atapadandia,gari moshi la mtoni
Asievishwa kilemba,hawezi kufunga domo.


5.Cha ukoka kikosea,cha gomba atatamani
Cha kuti atamendea,ajione wa thamani
Cha mbuyu kuotea,siyo bingwa wa barani
Asievishwa kilemba,hawezi kufunga domo.


SHAIRI-ASIEVISHWA KILEMBA
MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
Asante kwa ushairi...! Na mimi ni'mevamia' fani ya ushairi. Nitaomba msaada wako ili niweze kuwa bora katika kada hii.
====
Nikirudi kwenye mada; kwa sababu ya ugeni kwenye fani hii ya ushairi; tafadhali niomba ushauri namna gani bora ya kuujadili ushairi hapa jukwaani?
 
Njia bora kabisa ni kufuata kanuni na sheria za Jf zilizowekwa ambazo zitasaidia kujadili NA HATA kuweka mashairi humu bila kuwakwaza wengine.
Japokuwa bado sanaa hii haijulikani sana na wengine lakini tunajitahidi kadiri ya uwezo wetu kuhakikisha inawafikia wengi na kupendwa zaidi.
 
Back
Top Bottom