Asikwambie mtu baba Yanga Tamu!

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Pamoja na kundi la upande wa pili jana kusubiria kwa hamu kutwa nzima ya jana eti yanga ingeenda kupoteza mchezo ..hali haikuwa hivyo...yanga kakimbiza mwanzo mwisho. Watu tume enjoy burudani safi ya kandanda..

Umiliki mpira na talents za hali ya juu, tutoe pongezi kwa wachezaji wote benchi la ufundi kwa kutupa raha. Kwa upande wangu nikiri kwa umri wangu tokea nimeanza kuwa na utambuzi wa mambo ya soka sikuwahi kuiona yanga imara na ya kuvutia kiasi hiki!

Hongereni sana wananchi popote pale mlipo...hongereni sana wachezaji na benchi la ufundi.

Hakika Yanga hii tamu jamani.
 
Hivi ndo Vitu wanamsimbazi Wamekuwa wakiinjoi takribani kipindi cha miaka mitano iliyopita na Ubingwa mara nne mfululizo Wakati huo Wana Yanga mlikuwa Mnafanya Maandamano ya Kwenda 'Airport' Kupokea aidha timu pinzani au Yale Magarasa yenu kipindi kile.

Sasa tunasema welcome to the 'game'.

Msikate Pumzi.
 
Malizeni kufukuzana kwanza, makombe mengine yaandikeni majina kamili ya Makonda
 
Yanga ya msimu huu kuna timu zitagoma kuingia uwanjani.
Mudi fc wanatamani kuhamia ligi ya Zanzibar! Maana msimu huu watachezeshwa Ndombolo ya Soro mwanzo mwisho!

Yaani Bamutu ba Congo habacheki kabisa na kima! Wapi Papaa Mayele, mutoto ya TChishekedi!! Wapi Papaa Makambo! Papaa Bangala! Papaa Moloko! Papaa Mukoko! na Papaa Mwinyi Zahera Mzee wa 'Boo'!! 😁
 
Tuzidi kuwaombea Wananchi. Lakini tusiwadharau wengine. Wahenga walituasa " Ukijisifu kwa mbio, msifu na anayekufukuza"

Yanga haijafika Bado safari ni ndefu. Tujifunze kuheshimiana. Ala moja haikai panga mbili.
 
Wanawaza watuibie nan wanaishiwa pozi
 
Tumechi 4 tu yani 4 tu mnajiona mabingwa hahahhahahaha yaani nawaonea huruma maana mtalia na kusaga meno ubingwa msahau
 
Jiandaeni kung'oa viti safari hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…