Asili, koo, desturi na utamaduni wa wangoreme

Cendy

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2015
Posts
1,250
Reaction score
2,309
Kabla ya yote napendakuwashukuru wote wazee wote waliotoa mchango wao wa mawazo, pia namshukuru mzee mkare MNyigana kwa kutumia mda wake mwingi kuandika hili chapisho
Kabila la wangoreme limeundwa na watu waliotokea Arusha, Kenya na watu wa kusini mashariki ya tarafa ya ngoreme kufatana na historia iliyopatikana watangulizi wa kuingia ardhi ambayo sasa inaitwa ngoreme ni watu wa ukoo wa wamaare waliotokea Arusha wa kabila la wasonjo. Badae walifatiwa na watu wa ukoo wa wataboori pia kutoka Arusha wakiwa na koo mbili za waihindi na wabugasa na asili yao walikuwa wawindaji zaidi .
Kundi la pili lilikuwa watu kutoka Kenya wengi wao wana asili ya kikurya kwa vile walipitia ukuriani. Koo za watu hao zilikuwa kama zifatavyo;
  • Wagiseero waliotokea Gisero Kenya na waliamini chui
  • Wagoosi waliotokea Goosi , Kenya
  • Wagitare walitokea Geitare Kenya
  • Wairegi kutoka Bwiregi kaskazini mwa mto Mara
Koo zingine kutoka eneo hilo ni za wa
  • Wabusawe
  • Wasweta
  • Waraguuri
  • Watimbaru
  • Wanyabasi
Kundi la tatu ni watu waliotokea ikizu ambao walikuja kuunda koo za wagimenye na wabwiro.
ASILI YA WANGOREME NA UHUSIANO KATI YA WANGOREME NA WAIKOMA:
Chanzo kingine cha habari kinaeleza kuwa waanzilishi wa kabila la wangoreme ni shujaa aliyeitwa Magwesi aliyetokea Regala Sanjo karibu na Loliondo.
Magwesi aliyekuja na damu ya kimasai waliokuwa wanaitwa Sonjo. Mtatiro Nyigana Mkare aliwahi kufika Sonjo na kuelezea kuwa wasanjo wana lugha inayofanana na lugha ya kingurimi kwa maneno mengi
Mzee magwesi aliamua kuhama Regata na mkewe na kwenda sehemu itwayo Manyare. Alipokuwa Regata alifanikiwa kupata watoto aliyekuwa wa kiume wa kwanza akamwita Waudira wa pili wa kiume pia akamwita Mwikoma na motto wa tatu Mogosuhi aliyekuwa wa kike. Ukoo wake ulizidi kupanuka akiwa manyare na alifia eneo hili hili
Baada ya Mzee Magwesi kuaga dunia aliwachia madaraka mwanae Wandira ambae aliamua kuhamishia familia yao sehemu ya kijito itwayo Manchira. Inaasemekana mwikoma alipenda sana sehemu hiyo ilikuwa na wanyama wengi kwa vile alikuwa mwindaji. Ndio maana waikoma wako eneo hilo hadi sasa wakiwinda.Hata hivyo Wandira aliyekuwa mkulima hakupenda sehemu hiyo ya manchira kwa vile kulikuwa na wanyama wengi walioharibu mazao yake. Kwa hiyo Wandira aliamua kuhama na dada yake Mogosuhi na kumwacha mwikoma Wandira alihamia ikorongo akiwa na watoto wengi akiwemo mkubwa aliyeitwa motto mkubwa aliyeitwa Sabayaya
Baada ya Wandira kuaga dunia sabayaya alishika madaraka ya familia naya sabayaya alipata watoto wengi akiwemo mtoto wake mkubwa aliyemwita Mongoreme. kijana mongoreme aliyeshika madaraka alikabiliwa na matatizo mengi likiwemo tatizo la kushambuliwa na wamasai mara kwa mara na hivyo kuamua kuhamia sehemuambayo angetengeneza kinga dhidi ya maadui obori. Sohemu hiyo ilikuwa ni bonde lilozungukwa na vilima vine vya magange, kibairemera, nyangekenge na kewaigenga ambapo ilikuwa ni rahisi kuziba milango mitatu iliyopo naye Mugusuhi alihamia Kenya na kuolewa huko.

Mangwesi

Mwaikoma
Wandhira
Mogusuhi
Sabayaya
Mongoreme
Msaai

Kwa watu wenye umri mkubwa bila shaka waliwai kusikiamisemo kama vile “Isabayaya ne wandira” wakiwa na maana kuwa Isabayaya mwana wa wandira na pia “Ngoreme ya Isabayaya” wakiwa na maana Ngoreme mwana wa Isabayaya. Aidha kuna matumaini yaliyokuwa yakisikika kama “Ngoreme wa Nyahaba” ikiwa na uwezekano kuwa nyahaba huyo alikuja baada ya Mongoreme
13.2 KOO, MILANGO YA WANGOREME NA ALAMA ZAO ZA KUAPIA
Baada ya kuzaliana na kuongezeka wangoreme waligawanyika katika milango mbalimbali na kuwa na alama za kuapia kama ifatavyo
I, Wagoosi kutoka Kenya kupitia ukuriani – Ng’ombe na brashi
Ii, Wagisero kutoka gisero, ukuriani – Ng’ombe
Iii, Wabugasa kutoka sanjo – Fisi
Iv,
Waihindi kutoka sanjo – Fisi
V,
Wamaare kutoka sanjo Sanjo – Ng’ombe na Nyani
Vi,
Wagitare kutoka gitare – Samaki
Vii, Wabwiro kutoka ikizu –Makoome Na kunde
Viii,
Wairegi kutoka Bwiregi- Ng’ombe Na Nyama
Ix ,
Wagimenye kutoka ikizu
X, Wanguku kutoka umasaini – Sarota
Xi,
Wabusawe
Kama ilivyoelezwa hapo awali, milango au makundi mengine yaishio ngoreme ni ya wasweta waraguuri, watimbaru na wanyabasi. Kwa upande wa arama watangulizi (wazee) wangoreme waliziweka ili yeyote atakayeapa kwa uongo mji wake upate matatizo.

13.3 Makundi Ya Kishujaa Ya Wasaai Na Wachuma
Wangoreme pia waligawa koo zao kwa makundi mawili katika kuashiriaushujaa. Makundi hayo ni Wasaai kutokana na jina la mtoto wa kiume wa mongoreme aliyeitwa masaai
Wasaai Wachuma
Abagisego Abarimbare
Ababugasa Abagaasi
Ababusawe Abairege
Abagitare Ababwiro
Ababutacha Abaihindi
Abamare Abanguku
Abagimenye Abakombo
Abaraguri
13.4 Makundi Ya Kirika
Kulikuwa na makundi mengine ya kirika ambayo kwa kingoreme yalijulikana kama amakora. Rika hizo kwa upande wa Wasaai na Wachuma ni kama zifatazo
Wasaai Wachuma
Abasaai Abachuma
Abamaina Abanyangi
Abagamunyari Abagini
Abanyambureti Abamairabe
Rika hizo zilienda Kwa mzunguko moja baada ya mwingine kwa mfano Abachuma mzunguko upo kama ifatavyo.

Abachuma Abanyangi

Abamairabe Abagini

Pia kulikuwa Na makundi mengine yanayojulikana Kwa lugha ya kingoreme Kama Chisaga Kama ifatavyo

Wasaai walikuwa na “chisaga” za Bongirate na Romore
Wachuma walikuwa na chisaga za Borimarancha na Gamuntenya.

13.5 Miezi ya Wangoreme
Hapo zamani wangoreme hawakuwa na utaratibu wa kuhesabu miezi kama ilivyo siku hizi yaani Januari, Februari……… Hadi Desemba. Badala yake waliweza kuhesabu miezi yao kufatana na majira ya kilimo kama ifatavyo
1, Itaturi—Matorora (Mashamba yaliyovunwa)yanaanza kuota majani (yaraitaroora)
2, Itabarari --- wawindaji wanawinda
3, Kimaga – mwezi ambao mvua hainyeshi, kwa hiyo unawake kwa uwazi zaidi
4, Kemwamuya ya mbele (I)—Mwezi unakuwa mweusi kwajili ya kutanda mawingu ya mvua.
5, Kemwamu ya kabere (II) ---
6, Kirabu (I) ---Mvua nyeupe sio nzito
7, Kirabu (II) ---- kwendelea kwa kirabu
8, Nyamabeho --- Mwezi wa baridi
9, Nyansahi – Mwezi baada ya mvuno, sherehe, saro, kutembeleana
10, Rungaka—Mmea aina ya “rugaka” umeanza kutoa maua.
11, Tiiri – Kilimo kuanza na kupanda mazao
12, Kinyariri --- Majani yaliyochomwa yanaota upya

  • Utawala wa Wangoreme
  • Kwa kawaida wangoreme walikuwa hawana utemi wa kimila ila kulikuwa na utemi wa utawala. Kabla ya watemi hao wangoreme walitawaliwa na Wakora Nyangi ambao walimaliza matatizo yote na waliogopwa sana. Watemi ambao wametawala ngoreme tangu Mjeremani ni kama ifuatavyo:
  • Mtemi Kichamri na Mairo Ichumbe (1932 – 1936)
  • Walitawala ngoreme kwa awamu moja yaani kila mtu na eneo lake. Kichamri alitawala eneo la Mwibara na Mtemi Mairo alitawala maeneo yote ya kando ya Mto Mara kuanzia Bumare hadi Borenga.
  • Watemi hao walikuwa na sifa zifuatazo:- Mtemi Kichamri alipenda sana utukufu yaani yeye alikuwa anabebwa. Na Mtemi Mairo Ichumbe alikuwa msafi, lakini anayesisitiza taratibu zifuatwe kwa hali ile Wangoreme hawakumpenda hivyo liliundwa kundi la siri ambalo lilimhamisha kwa nguvu na kwenda Ikoma na kufia huko.
  • Mtemi Birage 1936 – 1937
  • Huyu alikuwa mtu mwenye nguvu na mnene sana, inasemekana aliweza kushikiria L/Rover na ikashindwa kuondoka, lakini hakusoma hata kidogo. Alidanganywa na Atanas na kutia dole gumba kwenye barua ambayo ilimuondoa madarakani bila kujua.
  • Mzee Birage alitaka kupambana na Mzee Nyigana kwa mieleka, kabla ya zoezi hilo wakapewa jaribio la kula vyakula mbalimbali, hapo ndipo Mzee Birage alipoonyesha kuwa atamuumiza Mzee Nyigana kwani kibuyu cha togwa alikunywa chote bila kupumzika, ugali kisonzo alimega mara tatu akamaliza ugali uliomo. Hapo washauri ndipo walipozuia zoezi hilo.
  • Mzee Birage alifanana na mtoto wake wa kike kwa nguvu, urefu na unene bahati mbaya mama huyo alifia huko Ikizu.
  • Mtemi Athanas 1937 - 1947
  • Yeye alikuwa siyo Mongoreme alikuwa Mkwaya aliletwa Ngoreme kama Karani wa Mtemi Birage. Kwa kuwa yeye alijua kusoma na kuandika alifanya mapinduzi ya ujanja. Aliandika barua kwa Bwana shauri wa kikoloni akieleza kuwa Birage amesema yeye hawawezi Wangoreme na hawezi kukomesha wizi hivyo afadhali Atanas ashike madaraka ya utemi. Na kweli barua hiyo ikakubalika, na D.C akaja na kumtangaza Atanasi kuwa Mtemi.
  • Baada ya Mtemi Atanas kusimikwa utemi kweli alifanya kazi nzuri sana kweli alikomesha wizi, lakini kwa mateso makali sana kwa wananchi, mtu aliyehisiwa alipewa karai la kokoto au changarawe atafune kwa meno yake na alishinda juani. Pia alianzisha Amini (ekehore) ambayo ukihisiwa mwizi unawekewa maji yaliyochanganywa na dawa ndani ya fuvu la kichwa cha binadamu aliyekufa kwa ukoma. Baada ya mateso hayo ya muda mrefu na wizi kukomeshwa wananchi wengi walijenga chuki kwa Atanas hivyo kama ilivyokuwa kwa Mairo Ichumbe, Atanas naye aliundiwa kundi la siri ambalo liliongozwa na Nyamang’we Mayengo ambaye wakati huo alitoka vitani Burma mwaka 1947 Mtemi Atanas aliingiliwa na karibu vijiji vyote na kuhamishwa kwa nguvu kwenda Musoma. Baada ya kufaulu hilo wangoreme walikutana na D.C akisisitiza kuwa Mtemi Atanasi arudi lakini wangoreme walikataa na kusema yeyote watakayemleta nje ya wangoreme (kabila jingine) wao watamhamisha kama walivyofanya kwa Atanas. Baada ya D.C kuona hivyo alikubaliana nao na kuwataka wataje mtu toka kabila la wangoreme, wakatajwa watu wawili Simeona Nyichomba na Nyamang’we Mayengo walimchagua Simeon ambaye wakati huo alikuwa ni karani wa Mahakama huko Nyahuburi Tarime akashinda na kuwa Mtemi.
  • Baadaye kwa kuenzi kazi ya Nyamang’we Mayengo ya kuandaa mkakati wa kumng’oa Atanas wangoreme walitunga wimbo ukisema “Nyamang’we hee, Nyamang’we hee niye wakona eniko ikagi gwita omukama” kwa tafasiri Nyamang’we, Nyamang’we wewe ndiye uliyeunda kundi la siri kwenda kuua Mtemi.
  • Huo ndiyo ukawa mwisho wa utawala wa Mtemi Atanas ambaye alikuwa na mke wake aliyefahamika kwa jina la Tekela (Tecler). Ndiye aliyejenga shule ya Majimoto na Mahakama ya Majimoto. Pia kitu ambacho kiliongeza chuki kwa wangoreme dhidi ya Atanas, ni pale Atanas alipoiba fedha za makusanyo (Ekehenda) na kusingizia watu fulani fulani kuwa wao ndiyo wezi. Serikali ilipotuma mtu aitwaye Chonachona (Mnusaji) wakati anaelekea kwa Chacha Mwirabi ambako pesa hizo zilifichwa, Mtemi Atanas alimkemea Chona na kusema hili halina uwezo wa kunusa na hivyo kumrudisha Majimoto bila mafanikio ya kupata hizo fedha.
  • Mtemi Simeon Nyichomba 1947 – 1963
  • Huyu ndiye mtemi aliyetawala kwa kipindi kirefu na aliyependwa sana na watu alikuwa siyo mkandamizaji, ila alipenda rushwa yeye alikuwa anasema wazi kuwa “ARABA TARENTA RIKUMBATI“Tafasiri ndugu yangu lete tumbaku” na kesi inamalizika. Alileta sana maendeleo kwani katika kipindi chake shule, zahanati Marambo na barabara vilijengwa.
  • Zahanati: ya kisaka 1948, Majimoto 1947 na Kemgesi
  • Shule: Kisaka, Nyagasense, Nyiboko, Nyabehore na Kemgesi
  • Barabara: Toka Sirorisimba hadi Nyiboko.
  • Marambo: Nyiboko, Borenga, Buchanchari, Nyamihangate, Nyansurumunti, Nyabehore, Mwimwamu na Kemarambo/Kikora
  • Mtemi Simeon aliwapenda sana watu wake na yeye kupendwa sana. Baada ya sheria ya kufuta vyeo vya Ma – Chief na kutungwa. Mtemi Simeo alikuwa miongoni mwa watemi waliostafishwa na hapo kuwa mwisho wa utawala wake, alifariki 1964 akiwa ameoa wanawake wanne ambao ni Mkami Mahende, Nyambori, Kimori na Nyamang’ondi. Mtemi Simeon alikuwa na mwandiko mzuri sana, hata sasa yako katika makitaba ya chuo kikuu cha DSM, chumba cha kumbukumbu (Special Reserve). Mtemi Simeoni alikuwa akipita na kuwakuta watu husimamisha gari lake aina ya L/Rover na kuwasalimia, na watu hao walimnyenyekea sana, wakipokea salamu zake kwa kusema “Kasinge, kasinge, neku ntigeoho” “Tafasiri Mkuu, mkuu nife mimi kabla ya wewe”. Jina kamili la Simeon ni Simeon Clement Mapesa Nyarang’anya.
 
Safi sana

Historia safi sana hii, imenifanya nikumbuke mnada wa Masinki na maeneo ya Kenyamonta, Maburi na Kisaka.undefinedundefinedundefinedNgoja niisevu nipate cha kubishana kijiwe cha Wangoreme pale Nyasho mitumbani Musoma
 
Nzuri hiyo mkuu karibu kisaka
 
Back
Top Bottom