Mwanza inatokana na jina la Ng'wanzalima,mfugaji alieishi nera/machemba hivo basi kutokana na tabia ya qasukuma ya kufupisha majina walikuwa wakimwita ''ng'wanza" kwani usukumani kama we ni YOHANA wanakuita YOHA,MOHAMED utaitwa MOHA au MED kwa kuwa kulkuwa na mwalo kamanga wa kuvukia na mwalo nera wa kuoga na kunyweshea mifugo wakoloni walipofika wakaamua kuweka makao maeneo ya kwa Ng'wanza[lima] ikaanzia hapo kuitwa Ngw'anza ila kutokana na wajerumani kushindwa kuitamka na kuiandika Ng'wanza wakawa wanatamka 'mwanza' ambayo ipo hadi leo,pia kwa kuongezea tu wasukuma hawaiti mwanza bali huita NG'WANZA labda wakiwa wanazungumza kiswahili ndo hutumia jina mwanza