Baba Kisarii
JF-Expert Member
- May 7, 2024
- 1,844
- 3,089
Katika kipindi cha kabla ya enzi ya ukoloni, na hata ukoloni ulipoingia nchini Tanganyika, aina hiyo ya magari ndio yalikuwa vyombo vikuu vya usafiri nchini.
Magari hayo hayakuwa ya kuwasha kwa funguo (ignition key/starter). Yaani yalikuwa yanawashwa kwa kuzungusha "hendeli" kwa mikono....😀
Ukiangalia picha kwa makini ama ukizoom, unaweza kuona kuna kimtalimbo ambacho kimechomoza kwa mbele, chini kidogo ya taa. Kwa hivyo ili kuwasha injini ilibidi uzungushe hio hendeli kwa dakika kadhaa, kama wafanyavyo wasaga unga katika mashine za kusagia za kizamani.
Wakati huo kulikuwa na vijana wa kiume wenye msuli kidogo ambao ndio waliokuwa wakifanya kazi hiyo.
Na dereva, aghalabu alikuwa mzungu, akishaingia ndani ya gari alikuwa anampigia kelele kijana wa kuwasha gari: "OK! Turn Boy! turn boooy!! Yaani zungusha (hendeli) kijana! Zungusha kijana.
Nasi Wamatumbi kama ilivyo kawaida yetu tukisikia neno lazima tulitohoe kivyetu. Hivyo hata baada ya magari ya kuwashwa kwa hendeli yalipotoweka na kuja ya kuwasha kwa funguo, hadi leo msaidizi yeyote wa dereva, hasa wa lori, anaitwa "Tandiboi" ikimaanisha "Turn boy".