kiswahili n uzalendo,
kukizungumza n unadhifu
kukisoma n ushujaa
kukienzi ni uadilifu
kukisifu ni uhodari
kukidumisha ni umahili
kukieneza ni ukombozi.
kiswahili ni uzalendo,
kukidharau ni uhafidhina
kukitusi ni ubarazuri
kukibeza ni uzuzu
kukitokomeza ni uozo
kukisahau ni ushenzi
kukitelekeza ni uhayawani
kutokukisoma ni ufisidi.
shime waswahili
Dumisheni tunu hii
Iwafae maishani
Iweni nyinyi
watu wenye fikra njema
mkapate mema yake
mkashuhudie.