Asilimia 40 ya Madini Yanatoka kwa Wachimbaji Wadogo Lakini Maisha Yao Hayaakisi Wanachozalisha

Asilimia 40 ya Madini Yanatoka kwa Wachimbaji Wadogo Lakini Maisha Yao Hayaakisi Wanachozalisha

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MASACHE KASAKA - 40% YA MADINI YANATOKA KWA WACHIMBAJI WADOGO LAKINI MAISHA YAO HAYAAKISI WACHOKIZALISHA

Mbunge wa Jimbo la Lupa tarehe 27 Aprili, 2023 akichangia bajeti ya Wizara ya Madini ya Shilingi Bilioni 89.3 iliyosomwa Bungeni na Waziri wa Madini Mhe. Dkt. Dotto Biteko amesema Asilimia 40 ya Madini nchini yanatoka kwa wachimbaji wadogo.

"Pamoja na kazi nzuri inazozifanya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) lakini inapata bajeti ndogo sana. Tukiwekeza katika utafiti, wachimbaji wadogo watafanya shughuli zao kwa uhakika wakijua nini watakipata chini kinyume na sasa wanafanya uchimbaji wa kupiga ramli" - Mhe. Masache Kasaka, Mbunge wa Jimbo la Lupa

"STAMICO inachangia katika uzalishaji wa umeme kupitia makaa ya mawe, tunaisadia vipi STAMICO huku tuifikiria miaka 10 ijayo uzalishaji wa umeme kupitia makaa ya mawe ufikie MW 10,000 hadi 15,000. Ni jambo linalowezekana tukiwawezesha tu STAMICO" - Mhe. Masache Kasaka, Mbunge wa Lupa

"Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limekuja na mkaa rafiki, mkaa huu utakuwa ni mbadala wa mkaa unaotokana na miti, nashauri STAMICO wauze teknolojia hii ya kuzalisha mkaa rafiki kwa taasisi nyingine kama SIDO, VETA ili waweze kuipeleka kwa wananchi" - Mhe. Masache Kasaka, Mbunge wa Lupa

"Serikali iliangalie sana Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), linaweza kutekeleza miradi mikubwa na ya kimkakati na uzalishaji ukaongezeka na hatimaye uchangiaji katika pato la Taifa ukawa mkubwa zaidi" - Masache Kasaka, Mbunge wa Jimbo la Lupa wilayani Chunya

"STAMICO wamefanya kazi nzuri sana, wametoka kuwa shirika mfu hadi na hata kutaka kufutwa na ilifika hatua hata mishahara walishindwa kulipa lakini sasa wamepiga hatua na hata kuweza kuzalisha faida ya zaidi ya shilingi bilioni 70 kwa mwaka" - Mhe. Masache Kasaka, Mbunge wa Lupa

"Kodi zinazomkabili mchimbaji mdogo ni nyingi sana hali inayopelekea anazalisha kwa wingi sana lakini tija anayopata yeye mwenyewe ni ndogo sana, naomba serikali mkae na kuona namna iliyokuwa bora ya kumpunguzia kodi mchimbaji mdogo" - Mhe. Masache Kasaka, Mbunge wa Jimbo la Lupa-Chunya

"Maisha ya wachimbaji wadogo hayaakisi kile wanachozalisha kwa sababu ya kodi nyingi na ada mbalimbali wanazotozwa, baada ya mfumo wa uchimbaji kuwa mzuri, taasisi za kimapato zinawaangalia wachimbaji wadogo kama chanzo cha kutafuta mapato" - Mhe. Masache Kasaka, Mbunge wa Jimbo la Lupa

"Wachimbaji wadogo wameendelea kuongeza uzalishaji na kuchangia katika pato la Taifa. Katika madini yote yanayopatikana, 40% yanapatikana kupitia kwa wachimbaji wadogo, lakini wachimbaji hawa maisha wanayoishi hayaakisi na kile wanachokizalisha" - Mhe. Masache Kasaka, Mbunge wa Lupa

"Wizara ya Madini imeendelea kukua mwaka hadi mwaka, na kwenye kuchangia pato la Taifa imeendelea kufanya vizuri, tuna imani ile mipango yake ya kufikia asilimia 10 ya kuchangia katika pato la Taifa itafikikiwa kwa wakati" - Mhe. Masache Kasaka, Mbunge wa Jimbo la Lupa wilayani Chunya

Fut1uZAWcAA9MOR.jpg
 
Hakuna wachimbaji wadogo Tanzania...hao wote ni vibarua.. wamiliki ni matajiri kina Laizer
 
Back
Top Bottom