Asilimia 60 chali matokeo ya kidato cha nne

Asilimia 60 chali matokeo ya kidato cha nne

lebraza

Senior Member
Joined
Jan 8, 2013
Posts
124
Reaction score
114
MATOKEO ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana yametangazwa. Watahiniwa 240,903 sawa na asilimia 60.6 wamepata sifuri, huku wanafunzi 23,520 tu ambao ni sawa na asilimia 5.16 ndiyo waliofaulu na wengine 103,327 sawa na asilimia 26.02 wamepata daraja la nne.

Akitangaza matokeo hayo jana, Waziri wa Elimu Dk Shukuru Kawambwa alisema watahiniwa walikuwa 456,137, wa shule wakiwa 397,136 huku wa kujitegemea wakiwa 68,806.
"Matokeo ya mwaka huu yamekuwa mabaya sana, Serikali tunasikitika kutokana na hali hii lakini tuna mipango mbalimbali ya kuhakikisha tunaweza kutatua hili tatizo," alisema Dk Kawambwa.

Dk Kawambwa alisema watahiniwa wote kwa ujumla waliosajiliwa walikuwa 480,036 kati yao wasichana 217,583 sawa na asilimia 45.33 na wavulana 262,453 sawa na asilimia 54.67 lakini waliofanya mtihani huo ni 456,137 sawa na asilimia 95.44, wengine 21,820 (asilimia 4.55) hawakufanya mtihani.

Alisema watahiniwa wa shule (school candidates) walikuwa 397,136 sawa na asilimia 96.57, miongoni mwao, 14,090 sawa na asilimia 3.43 hawakufanya mtihani huo kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo utoro, ugonjwa na vifo.

Ufaulu kwa madaraja
Kwa mujibu wa matokeo hayo, watahiniwa waliopata daraja la kwanza ni 1,641, wavulana wakiwa 1,073 na wasichana 568, daraja la pili ni 6,453, wavulana wakiwa 4,456 na wasichana 1,997.

Waliopata daraja la tatu ni 15,426, wavulana 10,813 na wasichana 4,613, waliopata wa daraja la nne 103,327, wavulana 64,344 na wasichana 38,983 huku waliopata sifuri wakiwa 240,903, wavulana 120,664 na wasichana 120,239.

Shule 20 bora
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wizara ilitaja shule 20 zilizofanya vizuri badala ya 10 kama ilivyozoeleka, kati yake 18 zilikuwa za watu binafsi na mashirika ya dini na mbili za Serikali.

Shule hizo ni pamoja na St.Francis Girls ya Mbeya, Marian Boys ya Pwani, Feza Boys ya Dar es Salaam, Marian Girls ya Pwani, Rosmini ya Tanga, Canossa ya Dar es Salaam, Jude Moshono ya Arusha, St. Mar's Mazinde Juu ya Tanga, Anwarite Girls ya Kilimanjaro na Kifungilo Girls ya Tanga.

Nyingine ni Feza Girls ya Dar es Salaam, Kandoro Sayansi Girls ya Kilimanjaro, Don Bosco Seminary ya Iringa, St. Joseph Millenium ya Dar es Salaam, St. Iterambogo ya Kigoma, St. James Seminary ya Kilimanjaro, Mzumbe ya Morogoro, Kibaha ya Pwani, Nyegezi Seminary ya Mwanza na Tengeru Boys ya Arusha.

Shule 10 za Mwisho
Kwa upande wa shule 10 za mwisho, iliyofanya vibaya zaidi ni Mibuyuni ya Lindi, Ndame ya Unguja, Namndimkongo ya Pwani, Chitekete ya Mtwara, Maendeleo ya Dar es Salaam, Kwamndolwa Tanga, Ungulu Morogoro, Kikale ya Pwani, Mkumba na Tongoni za Tanga.

Matokeo yaliyofutwa
Jumla ya watahiniwa 789 wamefutiwa matokeo kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na udanganyifu na kuandika matusi.

Baadhi ya udanganyifu huo ni karatasi za majibu kuwa na mfanano usio wa kawaida, kukamatwa na simu za mkononi kwenye chumba cha mtihani, kukutwa na karatasi au madaftari pamoja na kubadilishana karatasi za majibu.

Dk Kawambwa alisema matokeo ya watahiniwa 28,582 yamezuiwa kwa sababu ya kutolipa ada ya mtihani na wanatakiwa kulipa fedha hizo ndani ya mwaka mmoja.

Matokeo ya QT
Dk Kawambwa alisema waliosajiliwa kufanya Mtihani wa Maarifa (QT) walikuwa 21,310, wasichana 13,134 na wavulana 8,176 na waliofanya ni 17,137 sawa na asilimia 80.42... "Watahiniwa 5,984 kati ya 17,132 waliofanya mtihani huo wamefaulu."

source: Mwananchi leo
 
jamani nmejaribu kufanya utafiti ktk shule kumi bora kitaifa sijaona mwanafunzi aliyepata A ya History,najiuliza hili somo mtihani ulikua mgumu au ni umburula wa wanafunzi,au walimu wanawafundisha history ya india?
 
Wadau kuna tetesi kuwa baada ya matokeo ya form form 2011 yaliyotoka mwaka jana mwezi kama huu na kumuumbua mwanaasha jakaya kikwete, mwaka huu pia hali imejirudia baada ya watoto wengi wa mawaziri na vigogo wengine kuharibu vibaya katika matokeo hayo na hivyo kulishinikiza baraza kutoa matokeo kwa namba tu yaani bila majina! Source: kigogo mmoja wa NECTA ambaye ni jirani yangu.
 
teh teh kwani watoto wao c wanaxoma zile shule zinazoongozaga kitaifa au....teh teh kwel chenga n chenga tu itajtenga hata kwnye mchele tupu...
 
aisee kweli bhana! Nilikuwa sijajua kwamba ni mwanaisha kikwete kasabisha haya mabadiliko!
 
Wadau kuna tetesi kuwa baada ya matokeo ya form form 2011 yaliyotoka mwaka jana mwezi kama huu na kumuumbua mwanaasha jakaya kikwete, mwaka huu pia hali imejirudia baada ya watoto wengi wa mawaziri na vigogo wengine kuharibu vibaya katika matokeo hayo na hivyo kulishinikiza baraza kutoa matokeo kwa namba tu yaani bila majina! Source: kigogo mmoja wa NECTA ambaye ni jirani yangu.
siyo kweri wameogopa waislamu kulalama kufelishwa kama zanzibar ilivyotokea last year
 
Kwa matokeo haya ya 4m4 hivi elimu ya Tanzania inaelekea pazuri, au tunatoka pazuri kuelekea pabaya?
 
eti kila kufeli wanafunzi wanadai maabara hakuna?yaani kiswahili,english,history nayo haya masomo yanahitaji maabara?tuache visingizio jamani
 
Wasisingizie maabara maana wengi ni wasomaji wa arts hapo hakuna maabara labda biology pekee.
Lawama kwa serikali
 
Msisumbue vichwa walimu wanaionesha serikali uwepo wao na umuhim wao.

Si kweli kwamba wanafunzi hawana uwezo huo bali ubabe wa serikali, wanafunzi wanaumizwa na walimu.

Ni rahisi kumnyima mwanafunzi A wa history kuliko wa hesabu na physics kwasababu kisasi cha walimu kwenye masomo ya kujieleza kinabana wanafunzi kwenye small mistakes misspelling na grammar unachinjwa mpaka unatoka na D hatakama ulikuwa wa B.

Wakulaumiwa ni kawambwa na kikwete kushindwa kukidhi haja na maslahi ya walimu kama ilivyo kwa madaktari watu wengi wamekufa.
 
au kulikuwa na marking sceme tofauti? maana hata mitihani ya dini nasikia hazikuwepo ikabidi waandae nyingine...
 
pinda_sec.JPG
dr_slaaa.JPG
sumaye_sec.JPG
jk_kikwete.JPG
lukuvi_sec.JPG
regina_lowwasa.JPG
membe_sec.JPG
malecela_sec.JPG
dr_nchimbi.JPG
philimone_sarungi.JPG
dr_shein.JPG
salma-kikwete.JPG
cheyo.JPG
anaa_mkapa.JPG
 
Back
Top Bottom