pingli-nywee
JF-Expert Member
- Sep 16, 2015
- 11,923
- 13,350
Nimeshangazwa sana na hizi habari kuhusu mizigo ya Uganda ambayo huwa inapita kwenye bandari ya Mombasa. Baada ya kelele zote ambazo huwa nazisikia humu, kutoka kwa majirani zetu nilidhani kwenye biashara ya kupokea na kusafirisha mizigo ya Uganda, Kenya na Tz tungekuwa tunagawana angalau 50-50. Kumbe ushindani wa bandari ya Dar kwenye biashara ya nchi moja tu ambayo inapakana na nchi zote mbili za Kenya na Tz ni longolongo na porojo tu. Hawa jirani zetu nasikia ni mandugu wa kufa na kupona. Eti na mmoja wao aliikomboa nchi ya mwenzake kutoka kwenye minyororo ya udikteta. Kumbe miaka yote hii ikifika kwenye biashara Kenya na bandari yake ndio imekuwa ikifanya vitu vinavoeleweka? https://www.trademarkea.com/news/kenya-news/82-of-ugandas-cargo-passes-through-mombasa/