Asilimia 82 ya utajiri duniani unamilikiwa na asilimia 1 ya matajiri duniani

Asilimia 82 ya utajiri duniani unamilikiwa na asilimia 1 ya matajiri duniani

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
tajiri.jpg

Pengo baina ya matajiri wakubwa na watu wa kawaida lilipanuka zaidi mwaka jana kwa mujibu wa shirika la Oxfam.

Asilmia 82 ya fedha zilizotengenezwa mwaka jana zilikwenda kwa asilimia moja tu ya idadi ya watu duniani wakati maskini hawakupata ongezeko lolote la fedha, limesema shirika hilo.

Oxfam imesema takwimu hizi- zilizokoselewa na wakosoaji- ni ishara ya kushindwa kwa mfumo wa utawala duniani.

Limelaumu ukwepaji wa kodi, ushawishi mkubwa wa kampuni mbalimbali, kudorora kwa haki za wafanyakazi na kubanwa kwa matumizi kuwa chanzo cha hali hiyo.

Oxfam imetoa ripoti zinazoendana na suala hili kwa miaka 5 iliyopita.

Mwaka 2017 shirika hilo lilisema kuwa mabilionea wanane wanamiliki mali sawa na mali ya watu 3.6 bilioni kwa pamoja.

Mwaka huu imesema watu 42 wanamiliki mali sawa na nusu ya maskini duniani, lakini ikarekebisha idadi hiyo na kusema ni watu 61.

Shirika la Oxfam limesema marekebisho hayo yametokea kwa sababu ya maboresho ya takwimu na kusema mwanya kati ya walionacho na wasionacho umebaki hapo hapo.

Chanzo: BBC Swahili
 
Back
Top Bottom