TUMBIRI
JF-Expert Member
- May 7, 2011
- 1,933
- 1,199
Mhadhiri Mwandamizi wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Dk Honest Ngowi amesema ripoti ya utafiti uliofanyika hivi karibuni uliodhaminiwa na Shirika la nchini Norway (Norwegian Church Aid) imegundua kwamba asilimia 89 ya Watanzania hawalipi kodi kutokana na mfumo uliopo sasa katika ulipaji kodi uliojikita zaidi kwa sekta rasmi huku ikisahau sekta zisizo rasmi.
Katika ripoti hiyo imegundulika kwamba Mamlaka ya Mapato Tanzania imekuwa ikiwabana sana wafanyakazi wachache katika sekta rasmi ikiwaacha watu wa sekta isiyo rasmi ambayo ina watu wengi. Kwa mujibu wa utafiti huo Tanzania ina watu Milioni 15 kwenye sekta zote mbili (Rasmi na isiyo rasmi) ambao kimsingi wanatakiwa kulipa kodi. Lakini wanaolipa kodi ni Milion 1.5 tu tena wengi wao kutoka sekta rasmi huku 13.5 hawalipi ambayo ni sawa ya asimilia 89.
Source: Nipashe 08/09/2012 - Bofya hapa
TUMBIRI (PhD, University of HULL - UK),
tumbiri@jamiiforums.com