Asilimia 89 ya Watanzania hawalipi kodi

TUMBIRI

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2011
Posts
1,933
Reaction score
1,199
Mhadhiri Mwandamizi wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Dk Honest Ngowi amesema ripoti ya utafiti uliofanyika hivi karibuni uliodhaminiwa na Shirika la nchini Norway (Norwegian Church Aid) imegundua kwamba asilimia 89 ya Watanzania hawalipi kodi kutokana na mfumo uliopo sasa katika ulipaji kodi uliojikita zaidi kwa sekta rasmi huku ikisahau sekta zisizo rasmi.

Katika ripoti hiyo imegundulika kwamba Mamlaka ya Mapato Tanzania imekuwa ikiwabana sana wafanyakazi wachache katika sekta rasmi ikiwaacha watu wa sekta isiyo rasmi ambayo ina watu wengi. Kwa mujibu wa utafiti huo Tanzania ina watu Milioni 15 kwenye sekta zote mbili (Rasmi na isiyo rasmi) ambao kimsingi wanatakiwa kulipa kodi. Lakini wanaolipa kodi ni Milion 1.5 tu tena wengi wao kutoka sekta rasmi huku 13.5 hawalipi ambayo ni sawa ya asimilia 89.

Source: Nipashe 08/09/2012 - Bofya
hapa


TUMBIRI (PhD, University of HULL - UK),

tumbiri@jamiiforums.com
 
Safi sana ,si zinaliwa tu wAnataka tulipe na wao wailipe dorwans.shenzi.
 
Kwanini walipe wakati wengine wanapewa misamaha bila aibu,na wengine wanafisidi kwa hicho kidogo kinachokusanywa. Suala la kodi liwekwe kwenye katiba mpya na iwe ni kosa kwa mtu mwenye shughuli halali kutofanya hivyo.
 
Ndugu hata juzi nlikuwa arusha nikawa najiuliza kitu kama icho,mfano nliingalia ukitoka mjini arusha stend ya mabasi madogo ukapita sokoni kwa mguu,ukaja mpaka nazi ukaja mpaka mwisho njiro utakutana na nembo za makampuni zaidi ya elfu2 ndo nlizoweza kuhesabu kwa haraka,ila nlipoenda tra pale mapato house nlikuta rekodi ya makampuni isiyozidi 700 ambao wako active ktk ulipaji kodi...nikajiuliza ivi kweli taifa liko serious ktk kukusanya kodi?mfano pale tra arusha,tax collection officers hawazidi30 ndo wazunguke jiji zima katika kukusanya kodi?pale nje wameweka ubao umeandikwa HAKUNA KAZI,na angalia vijana wangapi wako mtaani hawana kazi?? Taifa linafanya siasa kwenye kila kitu! Our land is land of failed leadership and weakest governance!
 
TRA wamechapa usingizi
 
Ukiangalia kwa haraka haraka,wafanyakazi ndo pekee wasioweza kukwepa kodi. Mfanyakazi mwenye gros pay ya mil 1 hulipa zaidi ya mil kwa mwaka lakin mfanya biashara wa kulipa kodi ya mil kwa mwaka ni mwenye biashara ya ukwel! Tutafika tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…