JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Raia wa Afghanistan wamesherekea Sikukuu ya Eid, Mei Mosi huku wengi wao wakiwa na tatizo la njaa. Umoja wa Mataifa (UN) imeeleza kuwa zaidi ya asilimia 90 ya raia wa taifa hilo wanakabiliwa na uhaba wa chakula tangu uongozi wa Taliban uliposhika madaraka Agosti 2021.
“Nani atanipa fedha au chakula? Mji wote una njaa, sijawahi kuona hali kama hii hata tulipokuwa katika makambi ya wakimbizi ambapo ndipo nilipokulia,” anasema mkazi ambaye hakutaka kuweka wazi jina lake.
Kiongozi wa Taliban, Haibatullah Akhunzada alishiriki tafrija za Eid Jijini Kandahar amepongeza uhuru wa taifa hilo lakini hakuzungumzia haki za kibinaadamu.
Source: Aljazeera