Asilimia 90 ya wakazi wa Afghanistan wanakabiliwa na uhaba wa chakula

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607

Raia wa Afghanistan wamesherekea Sikukuu ya Eid, Mei Mosi huku wengi wao wakiwa na tatizo la njaa. Umoja wa Mataifa (UN) imeeleza kuwa zaidi ya asilimia 90 ya raia wa taifa hilo wanakabiliwa na uhaba wa chakula tangu uongozi wa Taliban uliposhika madaraka Agosti 2021.

“Nani atanipa fedha au chakula? Mji wote una njaa, sijawahi kuona hali kama hii hata tulipokuwa katika makambi ya wakimbizi ambapo ndipo nilipokulia,” anasema mkazi ambaye hakutaka kuweka wazi jina lake.

Kiongozi wa Taliban, Haibatullah Akhunzada alishiriki tafrija za Eid Jijini Kandahar amepongeza uhuru wa taifa hilo lakini hakuzungumzia haki za kibinaadamu.


Source: Aljazeera
 
Wapambane na hali yao, sasa wako huru hivyo hawana kisingizio sasa hiyo njaa inatoka wapi tena? Wachape kazi.
 
Haya waarabu wa buza ndugu zenu hao njaa inawakabili..watumie mihogo na mahindi wakale wasife njaa.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…