Asilimia 98 ya wasanii wapo chama tawala

Asilimia 98 ya wasanii wapo chama tawala

chizcom

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
8,680
Reaction score
18,035
Kuna kampeni inaendelea kumuangusha kijana Diamond kwenye tuzo za BET. Ukiliangalia naona limekuwa lenye upinzani ambao umeingiliwa na vyama vya upinzani kwa ajili tu siasa ziwepo sijui.

Sasa nauliza kama mtu Mwijaku wewe ulianza kwa ajili kumpiga chini mwisho likaingilia vyama vya pinzani.

Je, yeye akigombea tuzo za habari na yeye tupige chini maana yeye ni CCM.

IMG_6421.jpg

Tuje kwa wasanii wanaoshabikia mfano Alikiba na yeye ni CCM akipata tuzo hizo BET naye tupige chini !maana sera ya kupiga chini ni kwa sababu ya wasanii hawakemei maovu ndani ya chama chao kama vyama pinzani inavofanya.

IMG_6419.jpg

Kama mnaona uzalendo ni kugumu tunapoelekea sio pazuri
 
Kumbuka watanzania wengi walishakata tamaa na siasa hizi za kimabavu. Watu wana ulemavu wa kudumu uliosababishwa na hao makada
Sasa mtu ambaye wanamshabikia anapopita na kuwananga matokeo yake ndo haya
 
𝚂𝙸𝙼𝙱𝙰 𝚙𝚊𝚕𝚎 𝚔𝚞𝚗𝚊 𝙼𝚘𝚘 𝚗𝚒 𝙲𝙲𝙼 𝚜𝚒𝚓𝚞𝚒 𝚒𝚝𝚊𝚔𝚞𝚓𝚊 𝚗𝚊𝚢𝚘 𝚔𝚒𝚜𝚊 𝚖𝚏𝚊𝚍𝚑𝚒𝚛𝚒 𝚗𝚒 𝙲𝙲𝙼 𝚋𝚊𝚜𝚒 𝚝𝚞𝚙𝚒𝚐𝚎 𝚌𝚑𝚒𝚗 𝚂𝙸𝙼𝙱𝙰 𝚗𝚊 𝚝𝚞𝚏𝚊𝚗𝚢𝚒𝚎 𝚑𝚞𝚓𝚞𝚖𝚊 𝚒𝚜𝚒𝚌𝚑𝚞𝚔𝚞𝚎 𝚄𝚋𝚒𝚗𝚐𝚠𝚊?
 
Pale clouds FM ilikuwa ni kampeni mwanzo mwisho Hadi wengine wakapewa na U-DC

TBC ndio usiseme.

Millard Ayo ilikuwa ni mwendo wa kusifia tu.

Wasanii kalibia wote walimpigia kampeni Magufuli.

Mo alitekwa lakini alisema nini naye ilikuwa mwendo wa kusifia tu.

Wana-CCM kalibia wote hakuna aliyekuwa anauwezo wakusema lolote mbele ya Magufuli.

Mtoto wa tandale ndio angefungua mdomo wake hahahaa this is joking guys mtu Kama Kinana aliombeshwa msamahaa imagine Diamond angefanywa nini.
 
Jibu ni moja tu Diamond ni mkubwa zaidi ya Chadema,hivi kweli uhangaike na Ali KIBA,harmonize,millardayo si Unataka watoto wa watu wasiende chooni kabisa.

Madhara ya ukubwa ndo hayo anakutana nayo diamond sasa
 
Wacha Mond avune usaliti alioupanda kuungana na watesi kwa tamaa ya pesa.
 
Wasanii ni sehemu ndogo sana ya siasa za Tanzania. Kumwangusha Diamond bado hakuwezi kuiondoa CCM madarakani. Hao wakina Tundu Lisu wanaonekana jinsi gani wamepoteza mwelekeo. Kwanini wasianzishe petition watu tusaini kudai katiba kama wapinzani wa kweli? Badala yake wanapambana na watu kama Diamond, kweli wapo serious? Mimi siipendi CCM, lakini swala hapa, hata hao CHADEMA ni waganga njaa tu, ndio maana wananchi wanawaona magumashi tu. Watanzania sio wajinga.
 
Sisi konde gengi tunamshusha dimondi hivyo hivyo na huu upepo msituulize tupo chama gani🤸‍♂️🐒🤣
 
Viongozi wa dini maarufu na wakubwa jaribu wote wanashiriki mikutano ya ccm, inabidi wanaharakati uchwala waache kwenda kusali kwenye nyumba za ibada zinazosimamiwa na viongozi hao.
 
Nchi yetu bado tunapambana na maadui watatu

1 Ujinga
2 Umaskini
3 Maradhi
 
Back
Top Bottom