"Askari" aonekana akimwekea Davis Mosha kitu mfukoni

field marshall1

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2017
Posts
1,171
Reaction score
2,732
Nimeangalia kwa makini clip ya askari waliojifanya kuwa wa IMMIGRATION waliokwenda kwa Davis Mosha,Mmoja wa hao "maaskari" aliyevaa shati la kijivu alimsogelea kwa kumvizia Davis Mosha wakati wakibishana na hao "askari feki" akamuwekea kitu mfukoni halafu akamsukuma. Tumesikia kuwa Davis Mosha alipelekwa polisi.....Ninahisi kuwa aidha walimtilia bangi au Dawa za kulevya au simu waliyosema aliwanyang'anya wao. Aliyevaa shati la kijivu anafanana na yule aliyemtolea Nape Nnauye bastola mwaka jana.
Inasikitisha kuona nchi yetu inaharibiwa na hao askari wa Makonda. Huo ni mfano mwingine wa aina ya uvamizi unaofanywa na askari wa Makonda, ukianzia Clouds TV, Utekaji wa Roma Mkatoliki na uvamizi kwenye kituo cha mafuta cha Peter Zakaria huko mkoani Mara. Aina hiyo ya uvamizi na utekaji unafanana kwa namna moja au nyingine hivyo inaonekana mpangaji wa hayo maovu inawezekana akawa mtu mmoja ambaye si mwenye akili kabisa, Tumefikia pabaya kwa mambo yanayotokea nchini mwetu imekuwa kama Uganda wakati wa Idi Amin na Malyamungu walivyokuwa wakitumia vikosi vya State Bureau kuteka na kuua (au kupoteza watu....Kama anavyosema Jerry Muro) Hiyo link hapo chini utaona video yote. Kama utaclick na itashindwa kufanya kazi copy
 
Asante Field Marshall1,

Aisee, una macho makali sana. Nimeona, kwanza aliingiza mkono wake mfukoni, akautoa akiwa amefumba viganja, halafu kwa ujanja ukajifanya anamsukuma Mosha huku mkono ule uliofumbwa akiuingiza mfukoni mwa Mosha. Hakika huyu jamaa ni yule yule aliyemtolea Nappe bastola.

Mh. Sana Rais Magufuli, haya mambo yaendeko siko. Inawezekana unampenda sana Makonda, lakini mambo anayoyafanya kwa raia wako, yanaharibu kabisa sifa njema uliyo nayo na bidii yako ya kuwakomboa watanzania.

Pamoja na kuwa huyu umpendae anatumi watu wasiojulikana au usalama wa taifa, mwiso wa yote wewe ndiye amiri jeshi wa majeshi yote hapa nchini. Haiwezekani ukampenda sana mtu mmoja na kumwacha aangamize watanzania wengi namna hiyo kwa faida yake binafsi. Naamini watu wako wanasoma jamii forum na hivyo watakufikishia ujumbe huu.

Naandika haya kwa uchungu na kwa nia njema, lakini kama utaamua kuniangamiza na mimi pia, sina la kufanya kwani uamuzi ni wako. Lakini mwisho wa yote, sote tutakufa na kuiacha dunia hii. EE MUNGU NISAIDIE! Kilangila.
 
Nimeangalia Mara 17 but sijaelewa. Suruali ya mosha imembana saaana kuwekewa kitu so jambo rahisi
Ukiangalia kwa makini huyo mwenye shati la kijivu ametoa kitu mfukoni kwake akamsogelea Davis Mosha (Akajiweka upande kwa upande au kwa kiingereza "side by side" Kwa mkono wa kulia ambao aliufunga/aliukunja alipoutoa mfukoni mwake akaingiza kwenye mfuko wa suruali wa kushoto wa suruali wa Davis Mosha wakati huo akitumia mkono wa kushoto kumsukuma Mosha. Ukiangalia kwa makini mkono wa kulia wa huyo "askari"baada ya kuuingiza mfukoni kwa Davis Mosha akautoa ukiwa hauna kitu (Tofauti na mwanzo) halafu akatumia mikono yake miwili kumsukuma Mosha. Angalia kwa makini alichokuwa akifanya...kuwa "Detail oriented" Suruali kubana siyo tatizo kwa sababu si lazima alichowekewa siyo lazima kiwe kikubwa pia kumbuka hiyo suruali Davis Mosha anatumia hiyo mifuko ya suruali aidha kuwekea walet au inatosha pia kuweka mikono yake, hivyo suruali kubana siyo tija. Hapo yeyote mwenye macho na akili timamu anaona kilichotokea. Hapo ni simply kubambikiza....Hiyo system ya kubambikiza siyo ngeni hapa Tanzania hao polisi uchwara na polisi wa kawaida ni kitu wanachofanya siku zote. LINI HUU UONEVU UTAKWISHA?
 
Episode hii, inafanana sana na ile ya Zakaria yule tajiri wa Musoma. Kilangila.
 
Dah
Huyo jamaa ni nani mbona matukio yote ya ovyo yupo....
!?!?
Something is not right aisee.
 
Huyu ni npambe wa Mosha wala si askari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…