Hili neno limekuwapo tangu enzi za ukoloni. Maana yake, kama wachangiaji wengine walivyosema, ni askari anayevaa kiraia (njagu, jasusi, usalama wa taifa etc). Enzi za ukoloni ulikuwa unaweza kukuta jamaa kavaa kanzu na kibaraghashia kumbe jamaa ni askari (plainclothes officer) aliyepo kazini. Staili hii iliendelea hata baada ya uhuru ingawa nadhani siku hizi watu wengi hawatumii sana hili neno.