Wale wa JW mbona huwa hawapimi vifaru wanavyo safirisha?Unajua kifaru kina tani ngapi wewe?Kwahiyo ulitaka wawaachie waendelee kuharibu barabara kwakuwa wao ni askari,je ukiwa askari unahaki ya kuvunja sheria basi wote tuwe maaskari
Mbona una jikanyaka....kuna kila dalili hawajalipwa posho hivyo wana stress ndiyo maana wakaamua kuzimalizia kwa wahusika wa mizani...serikali imefilisika kuna walimu hawajaripwa mwezi wa tatu huu....Watakuwa wamelipwa posho kwa kukaa juani sasa wanakula viroba kwenye basi wapunguze stress sasa yamewakuta. Poleni masoldier!
Mkuu umenichekesha sana na swali jibu lako.....Wale wa JW mbona huwa hawapimi vifaru wanavyo safirisha?Unajua kifaru kina tani ngapi wewe?
CCM inahaki gani ya kufanyia mkutano wa chama Ikulu....Hivi wana haki gani kutoa kichapo na kuvunja samani wao ni kina nani wazuie sheria kufanya kazi au sheria ni kwa raia wanyonge tuu!!
Umeona eeeee, yaani hakuna tofauti!!Hiyo yote dugu moja
Hiyo yote dugu moja
Habari nilizozipokea hivi punde kutoka kwa mdau wangu wa mikoani kuwa askari magereza waliokuwa wakielekea Mbeya wakirudi wakitokea kwenye gwaride la muungano wamefanya vurugu kubwa kwenye mizani baada ya basi walilokuwa wamekodi la kampuni ya Muro kuwekwa korokoroni kwa kushindwa kulipa faini ya kuzidisha uzito,askari hao hawakutaka kuelewa wala kuruhusu wenye basi kulipa faini walianza kutoa kichapo kwa watu wa mizani na kuvunja meza,viti na samani hadi askari polisi walipoingilia kati kutuliza fujo hizo.Nawasilisha
hawajafanya vyema,sheria ifate mkondo wake