Superman nimekubali kweli unahisia...
Kwanza, mi naona wengi wa hao jamaa (askari) hawaamini kinachoendelea hapo, yaani kwa kifupi hawakutazamia msisimko mkubwa na mwitikio wa kimageuzi unaoonyeshwa na wananchi waliohudhuria hapo.
Pili, nadhani wanajaribu kutafakari ujasiri wa Rais mtarajiwa kwa jinsi anavyodiriki kuanika uozo wa serikali iliyopo madarakani bila woga. si unamuona yule mmoja kwenye gari la kulia ambaye hajavaa kofia jinsi alivyopanua mdomo na kutoa macho kwa kushangaa..
Tatu, nadhani wengi wao wanajaribu kutafakari kula yao itakuwaje baada ya Oct-31-2010.
Nne, nadhani kila mmoja sasa anaomba mungu wake ili matokeo yasichakachuliwe maana nguvu ya umma hawataweza kuikabili kirahisi .....