Askari Polisi aliyekuwa anatetea gongo bado ana kibarua chake?

Askari Polisi aliyekuwa anatetea gongo bado ana kibarua chake?

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
19,675
Reaction score
33,583
Wakuu,

Kama tunavyojua amri jeshi mkuu akitoa maelekezo huku chini ni utii tu. Mama Samia alioneshwa kukerwa na clip ya askari akifafanua mchanganyiko unaofanya gongo na kutetea mfumo/ process za utengenezwaji wake. Huku kukerwa ingawa sijadhibitisha inawezekana yule kijana hana kazi tena.

Nimeona majuzi tena mama yetu akikazia tukio lile. Kiukweli naona mama amelibeba kama tukio la ajabu sana na pengine hata huyo kijana kupoteza kibarua. Lakini nashauri busara zitumike kumpunguzia adhabu au kumsamehe huyo kijana ili atumikie taifa lake.

Tunayo mifano ya wazi ikiwemo wabunge tena wa CCM wakitetea bangi bungeni na hawakuonywa popote, tumeona gongo ikitetewa bungeni tena mara nyingi lakini halikutoka onyo lolote. Lakini huyu kijana mdogo clip ndogo imezima ndoto zake!

Nakuomba mama yetu Samia, msamehe kijana wetu! Pia tukio lile lisahau kidogo maana ulishatoa maelekezo. Kuendelea kulirudia ukiwa amri jeshi mkuu na kauli yako ni amri ni kuzidi kumuweka kwenye mazingira magumu.

Mama tafadhali fuatilia huyo kijana apewe nafasi nyingine! Rungu lako kwake ni zito sana, bora wenyewe maafande wapeane adhabu zao wanazozijua ikiwemo lock up ila maelekezo yako yanaweza kumshukia kama kupiga mende kwa nyundo.

Tumuombe Mh. Rais wetu amsamehe huyo kijana.

 
Yeye anauza Bandari huku akiwapinga wajasiriamali wa Viwanda! Gongo ni Pombe ambayo ilistahili kushikwa mkono na serikali kwa kupitia sido na TDMA na kisha kuwapatia Elimu wajasiriamali Gongo.

Ili iwe kwenye viwango vya Konyagi na Zinginezo. Badala ya kuwafunga Magerezani wataalamu hawa tangia Uhuru 1961.
 
Ifike wakati pia bangi ihalalalishwe na kutetewa ili wadau tuivute hadharani kwa uhuru tukitembea. Not walking looking over your shoulders.

adriz
 
Huyo askari mdogo asamehewe! Amejifunza kwa kosa hilo ...
 
Back
Top Bottom