Askari polisi wa uganda wakamatiwa tanzania wakiwa katika harakati za kuwakamata watuhumiwa wao..

Askari polisi wa uganda wakamatiwa tanzania wakiwa katika harakati za kuwakamata watuhumiwa wao..

makoye78

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2012
Posts
672
Reaction score
229
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, juzi tarehe 6.4.14, katika maeneo ya Mutukula (upande wa Tanzania), mpaka unaozitenganisha nchi za Tanzania na Uganda, kulizuka taflani ya aina yake baada ya askari polisi wapatao watano wa Uganda wakiwa wamevalia kiraia huku wakiwa na siraha za aina mbali mbali zikiwemo bunduki za kivita aina ya SMG na bastora, kulisanua kwa kutaka kukamata watuhumiwa wa wizi wa pikipiki katika nchi isiyokuwa ya kwao, kitendo ambacho ni kinyume cha sheria! Mlolongo wa tukio hilo ulianzia mjini Mbarara nchini Uganda, takribani kilomita 150 kutoka Mutukula, ambapo polisi hao wa Uganda walimkamata mtuhumiwa wa wizi wa pikipiki (mganda mwenzao) na kumtia kibano cha kutosha, kisha akawaelezea polisi hao ya kuwa huwa anaziuza maeneo ya Mutukula pikipiki zote aziibazo nchini Uganda. Kwa wasiojua, Mutukula ni mji mdogo ambao nchi zote mbili Tanzania na Uganda zinaugawana katikati!Walipofika Mutukula, wakiwa ndani ya gari lenye vioo vya tinted huku wakiwa wamesheheni siraha zao, aidha bila kujua ama kwa makusudi walivuka mpaka na kuingia Tanzania hadi kwenye kijiwe walichosontewa na mtuhumiwa wao waliyetoka naye Mbarara, ya kuwa mahali pale ndo huwa anauzia pikipiki baada ya kuziiba nchini Uganda!Kasheshe lilianza mara baada ya askari hao kuanza kurusha risasi hovyo hovyo, huku wakiwataka kuwa chini ya ulinzi watu wote waliokuwepo kijiweni hapo!Kibongo bongo, haikuwa rahisi kwa waganda hao kumkamata mtu kiulaini kwani vijana wote wa kijiweni pale walitimua mbio, mmoja akielekea kituo cha polisi cha Tanzania huku akirushiwa risasi na askari mmoja wa Uganda aliyekuwa akimtimua kwa mbwembwe za kivita, safari yao ikiishia Charge Room Office (CRO) au mapokezi ya kituo hicho cha polisi Mutukula Tanzania, ambapo wote wawili, walitiwa Mbaroni, huku Afande huyo wa kiganda akipokonywa siraha na maafande wa Tanzania, na kutiwa pingu, kisha sero ama lokapu kwa lugha ingine!Huko nyuma nako, wale maafande wanne wa kiganda wakinusurika kifo kwa kuzingirwa na raia wa Tanzania wakidai "hakamatwi mtu hapa", nao maafande hao, kunusuru uhai wao walimwaga mvua ya risasi na kufanikiwa kurudi Mutukula ya Uganda huku wakijeruhi watu wapatao wawili.Tutazidi kufahamishana kilichoendelea zaidi iwapo habari mpya zitapatikana, japo imeelezwa kuwa, askari waliotorokea Uganda walikamatwa na polisi wenzao wa Uganda, na inasemekana wote wamekwishakabidhiwa Tanzania!Zaidi, inasemekana ya kuwa, askari hao wote watano walijituma kazi hiyo, yaani ilikuwa deal yao tu, na wala uongozi wa jeshi la polisi nchini Uganda haiutambui kazi yao hiyo! Majanga....!
 
Kwanini hili bandiko liko jukwaa la sheria?
 
Kwanini hili bandiko liko jukwaa la sheria?
Mkuu, kwa jinsi nilivyoona, hapa kuna kesi ya kujibu inayowahusu askari hawa wa Uganda, nimeona habari hii niiweke hapa ili tukutane na wataalamu wa sheria tuweze kulijadili hili kwa mstakabali wa kisheria ili tujifunze zaidi nini sheria inasema katika hili! Ila kama bandiko hili hapa si mahali pake, basi mods wapo wanaweza kulihamishia kule kunakofaa!
 
Daata wewe ulitaka hili janga liwekwe jukwaa gani?Mi naona makoye78 yupo sahihi kabisa! makoye78 nakwambia hata maadui kutuingilia ni rahisi sana!
Mkuu LiverpoolFC, nashukuru kwa kuniunga mkono kuhusu jukwaa lipi bandiko hili liwekwe! Lakini pia hii iwe ni changamoto kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama hasa vilivyoko mipakani kuongeza umakini katika kuilinda mipaka yetu kwani kwa staili hii, ni kweli adui anaweza akaingia, akatutandika na akarejea kwake kabla hata hatujajua linaloendelea! Hii ni hatari kwa usalama wa raia na Taifa kwa ujumla!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom