Maafisa wa Jeshi la Polisi mapema leo wamefika katika msiba wa Sefu Mussa, mkazi wa Matejoo jijini Arusha, aliyefariki dunia baada ya kudaiwa kupewa adhabu na askari watatu wa Hifadhi ya Ngorongoro.
Sefu alidaiwa kufariki baada ya yeye na wenzake kupotea njia Aprili 12, 2026, walipokuwa wakielekea Babati kuhudhuria mazishi ya rafiki yao. Inadaiwa walijikuta wakiingia katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, ambako walikutana na askari hao.
Imeelezwa, kufika kwa maafisa hao msibani kunalenga kutoa pole kwa familia, pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama wakati wa mazishi ya Sefu, yanayotarajiwa kufanyika leo, Agosti 14, majira ya saa 10 jioni katika eneo la Mrombo.
Akizungumza kuhusu kifo cha mwanawe, baba mzazi wa Sefu amesema taarifa hizo zimemuumiza sana, huku akiitaka Serikali kuhakikisha haki inaten