Askari polisi wanne waliofanya mauaji ya kinyama Urambo warejeshwa kazini 'kimtindo'

kayogo

Member
Joined
Sep 15, 2010
Posts
75
Reaction score
42



HALI HALISI YA MAUAJI YA HASSAN MGALULA:

Askari Polisi hao wakati wakimchukua kwenye usafiri wa Bajaji ya mizigo huku wakiwa wamemkanyaga bila kujali hali mahututi aliyokuwanayo marehemu Hassan Mgalula mara baada ya kipigo kikali kilichosababisha kifo chake hapo baadaye,INASEMEKANA KUWA WALIPOFIKA KITUONI WALIFUNGUA JALADA LILILOONESHA KUWA HASSAN AMEPIGWA NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI......

POLISI wanne waliokuwa wanaodaiwa kuhusika na tuhuma za mauaji ya mtu mmoja huko Wilayani Urambo ambao walifukuzwa kazi baada ya kufikishwa mahakamani imedaiwa kuwa wamerejeshwa kazini huku yakizuka maswali mengi yasiyo na majiibu juu ya kuachiwa kwao.

Askari Polisi hao ambao walifukuzwa kazi mnamo March 5 mwaka 2012 baada ya kubainika wamehusika na tukio hilo la kinyama la kumpiga hadi kupoteza fahamu marehemu Hassan Mgalula ambaye baade alipoteza maisha ni namba G 3037 Pc Aidano, namba G 3836 Pc Jonathan, namba G 4836 Pc Mohamed na mwingine ni namba G 5382 Pc Khakimu.

Kuachiwa na kurejeshwa kazini kwa askari Polisi hao wanne kumezua hali ya sitofahamu kuanzia kwa askari Polisi wenzao hadi kwa wananchi wa wilaya ya Urambo ambao waliobahatika kulishuhudia tukio la kumpiga raia huyo wa Urambo marehemu Hassan Mgalula na baadae kufariki dunia kabla ya kufikishwa kituo cha Polisi ambako lilifunguliwa jalada kwamba ameuawa na wananchi wenye hasira kali.

Aidha juhudi za kumtafuta kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Athony Rutha ili kutolea ufafanuzi juu ya kurudishwa kazini kwa askari hao zinaendelea lakini kumekuwa na dalili za utata kutokana na askari hao imeelezwa kuwa kuna mikono ya vigogo wa Jeshi la Polisi ngazi ya juu.

Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Urambo kutokana na tukio la kurejeshwa kazini kwa askari hao wanaodaiwa kufanya unyama huo mnamo Februari 29 mwaka 2012 wameonesha dalili za kukosa imani na Jeshi hilo huku wakilalamikia uongozi wa Polisi ngazi za juu kwa kuendelea kuwabeba baadhi ya askari wanaotenda makosa kinyume cha sheria.
 
natamani siku nimkamate polis mmoja kwenye anga zangu...ndio maana wanatembea na wake za wenzao
 
Hii awamu ya Mr.Dhaifu ukiukwaji wa haki za binadamu nchini kwetu umekithiri sana.Watanzania Mungu tu ndiye aliyebaki mtetezi wetu.
 
Nasikia na yule aliyemripua matumbo Mwangosi alisikika akiwaambia waandishi habari waliokuwa wanajitahidi kupata picha yake kwamba ngojeni nitakapotoka. Tayari anajua kuwa atatoka.
 
Mbona Urambo hawapo? Au wamepelekwa vituo vingine? MUDI yuko Mbeya anaganga njaa na tumeongea nae leo hii anaendelea na mishemishe zingine tu na kama unabisha namba yake ya simu hii hapa muulize yuko wapi na anafanya nini saana atakwambia amemmiss DEMU wake wa Kisingida ambaye alikuwa polisi mwenzake aliyemwacha hapa Urambo, 0688822008
 
Sana Habari za ukweli kuhusu JESHI LA POLISI URAMBO ni kwamba aliyekuwa OC SIEIDY aliyestaafu mwaka jana Mzee CHIWANGO alishikwa na viungo vya ALBINO wakiwa na mwarabu mmoja anayeitwa SELE JIMY ila wako nje kwa dhamana
 
Jombaaa

Mi binafsi Sijaona cha maana chochote ulichosema....,kama watu wamepelekwa Mahakaman na baadae wakaachwa huru sasa we Unachoona cha Ajabu hapo ni kipi??? Maana Mahakama ndo ya kumtia m2 Hatiani....NDO MAANA HATUENDELEI TUMEKALIA MAJUNGU..,HAYO NI MAJUNGU
 

majungu vipi? jamaa alikuwa anauliza tu
 

Askari Polisi hao ambao walifukuzwa kazi mnamo March 5 mwaka 2012 baada ya kubainika wamehusika na tukio hilo la kinyama la kumpiga hadi kupoteza fahamu marehemu Hassan Mgalula ambaye baade alipoteza maisha ni namba G 3037 Pc Aidano, namba G 3836 Pc Jonathan, namba G 4836 Pc Mohamed na mwingine ni namba G 5382 Pc Khakimu

Mkuu hii sentensi (yenye red colour) uliisoma ukaielewa? au uliitfsiri vipi? read between the lines before you comment.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…