munisijo
JF-Expert Member
- Apr 10, 2012
- 1,126
- 942
Ni kweli, umuhimu wenu tunaujua lakini mbona faida yenu hatuifaidi katika ukamilifu? Toka nimekuwa na kumbukumbu, what I remember ni 'Kula, usipokula tunakuitia polisi' ... ni kweli nilikula lakini hadi leo nimekuwa mtu mzima na mwenye akili timamu, mtazamo wangu juu yenu umezidi kuwa hasi zaidi! Sina uhakika kama amani na utulivu tulio nao ni kwa sababu ya uwepo wenu ama utashi tu wa kibinadamu, sina uhakika pia uwepo wenu unaadhiri vipi kupungua/kuongezeka kwa uhalifu ... mara nyingine najiuliza, hivi mkipumzika kwa siku 3, ni kibaya kitatokea?!Yawezekana kisitokee chochote ...
Umaarufu mkubwa niusikiao juu yenu ni kuua, ndio kuua i.e Mwangosi, Mabwe-pande, Majambazi (Ingawa nasikia hairuhusiwi), rushwa , yeah, hapa sio siri mpo vizuri kwa kweli, uonevu, ubabe na matumizi ya nguvu yaliyopitiliza! Sifa nyingine kubwa mliyoipata ni kuthibiti maandamano ya vyama vya upinzani na kukitumikia chama tawala, ndio, kuelekea 2015 nitaendelea kutafiti nione kama tuhuma hizi ni za kweli...
Binafsi, nimekua na imani kubwa kwa 'Traffic Police', ukiacha wale wanaojificha kwenye vichaka na kushtukiza magari, wengi wa hapa mjini ni wachapakazi sana...hebu wafikirie wale wa pale Ubungo, Morocco, Magomeni ama Fire ... yeah, heshima kwenu, ni wabinadamu, wapole, mnaelimisha na kwa pollution ya Dar, MUNGU awalinde, kwa nyie wengine wa kitu kidogo naamini mtajirekebisha! Kundi jingine kubwa, bado jamii hatuja waamini vyakutosha hivyo ni vema mkaanza kujisafisha mapema before its too late .....
Hope anyone would want to prove me wrong, ni kweli, nimeshindwa kabisa kuwasifia askari polisi wengi only because hamtaki kutii viapo vyenu na kufuata sheria ... kama kuna yeyote mwenye ushuhuda mzuri ama mbaya wa askari polisi, karibia jamvini na utupe mtazamo wako kuhusu mada hii ......