Good Father
JF-Expert Member
- Feb 28, 2014
- 10,321
- 18,574
Wakuu leo asubuhi hii waliopita barabara ya Airport (Pugu road) ni mashahidi kuwa pana foleni ndefu kwa sababu ya misafara ya viongozi, awali alipita Makamu wa Rais, baadae kidogo kukawa na foleni kubwa na askari wengi sana barabarani bila shaka itakuwa IGP naye anatoka kwake Chanika kwenda Mjini.
Sasa kuna kisa kimetokea maeneo ya Mchicha pale kwenye njia panda ya kuingia barabara kubwa (Pugu road), mimi nilipanda bolt niwahi jambo langu, bolt alikosea njia tulikuwa tunatoka uelekeo wa airport kwenda Mchicha, ghafla trafiki huyu hapa ni mmama mtu mzima kama nimeona vizuri ni Staff sergeant wa polisi alikuwa na fimbo yake ya madaraka, yeye baada ya kuona boda amekunja pale alikasirika akarusha ile fimbo yake ili ampige dereva wa bolt.
Sasa nawaza kwa mfano ile fimbo ingempata dereva, pikipiki ikayumba tukapata ajali pale yule trafiki anahisi angekuwa salama?
Au ndio mafundisho mapya kwamba dereva akikosea bahati mbaya unapaswa kumpiga?
Nawaza tena, yule mama leo angekuwa na silaha ya moto angefyatua risasi kwa sababu dereva kakunja sehemu ambayo hairuhusiwi?
Polisi, Polisi, Polisi nawaita tena nawaambia tumieni akili, tumieni akili zenu.
We mama yangu trafiki uliyekuwa Mchicha leo kama tungepata ajali na nikasalimika nisife, ningefatilia vizuri nijue kama Serikali imekuchukulia hatua au la, kama ungeachwa mimi binafsi ningeshughulika nawewe nina hakika nakuweza vizuri tu.
Nawajua vizuri Polisi nje ya hiyo uniform hauna mtetezi, tumia akili zako vizuri maana wakati mwingine hata ukiwa na uniform ukishaharibu kazi wakubwa wako watakukataa.
Kwa muonekano ule wewe hauko mbali na kustaafu, linda hata hicho kipensheni chako.
Ni hayo tu..