Good Father
JF-Expert Member
- Feb 28, 2014
- 10,321
- 18,574
- Thread starter
-
- #21
Bodaboda tunawajua ndio maana hapa tunakusisitiza lawama zako zingeenda kwa bodaboda wako, na unatakiwa umripoti BOLT ili wamfungie... je, wewe unaweza kuikimbiza bodaboda ukiwa kwa miguu!? .... Ila ulitaka huyo askari mwanamama amkimbize na amkamate akiwa kwa miguu [emoji3][emoji3].
Hakuna anayekutolea povu instead tunakupa ukweli mweupe.
Don't take things personal ndugu.
Naona kuna wapumbavu wanatetea huyo Trafic. Sheria ni msumeno kila mtu afate sheria ndomana trafic wanapigwa.
Alirusha fimbo ili iweje sheria gani inamruhusu afanye hivi au kifungu gani inaamruhusu atende hivyo. Ndomana pale ubungu trafic alisimamisha lorry wakati lipo kwenye spidi likasimama ghafla bodaboda akafiriki akaivaa lory kama trafic sikukimbia wangemulia mbali wananchi.
Hakuna mtu anaeweza kimbia wakati usajili wa pikipiki unaonekana angemkamata na kumpa haki yake.
Mkuu hao ni askari ukiona wanatetea. Na haswa hawa wasio na vyeo tabaka la chini.Kuna watu hawaelewi hapa sijui ndo Polisi wetu wako humu au vipi.
Ni kweli bodaboda ametenda kosa la kukunja kona pasipotakiwa, mimi kama abiria sikuwa na taarifa wala sikujua kama angekuja pale maana ni ghafla tu.
Nimeshtuka naona jamaa anakwepa fimbo iliyorushwa ndio nikatambua jamaa kakunja kona mahali sio sahihi.
Ile reaction ya trafiki ilikuwa mbaya.
Madereva wanatenda makosa mara nyingi najua, lakini imegine ingekuwa gari alafu trafiki arushe fimbo ivunje kioo hizi arguments wanazoweka humu wangekuwa wao ndo gari imevunjwa wangesema huu utoto
Ni bahati tu hakijatokea kitu kibaya, mbona trafiki ningeenda mbele nikarudi kumkariri na kumsaka taratibu hadi nijue analala banda gani [emoji23][emoji23]
Bodaboda ni pasua kichwa,hawafuati sheria za barabarani,hawasimami kwenye stop,kwenye taa za barabarani.Wanaweza kukunja mbele ya gari,na kurudi anakotoka,bila kujali,wakiwasha pikipiki,hawatizami nyuma,kama kuna chombo kingine cha usafiri nyuma yake,anaondoka tu,yaani fujo tupu,kwenda mbele,wanapita njia za 'No entry makusudi.Wanasababisha ajali ovyo.Kuna ajali litokea,wamepakiana wanne,mmoja akalaliwa na bomba la moshi kwenye macho yote mawili,wengine waliumia vibaya.Nampongeza huyo mama trafick police,amejitahidi walau kumuonya kwa fimbo.Hakunaga kukosea njia bahati mbaya bro, assume kingetokea chombo kikingine ambacho kipo sawa mkapata ajali? Hao bodaboda usipowaongoza wana michezo ya kipuuzi sana barabarani!!
Halafu, bodaboda anaharibu makusudi abiria ndiyo anakuwa mkali kuhalalisha kosa la Dereva wa bodaboda!!