Askari wa barabarani wamepuuzia kutekeleza agizo la Makamu wa Rais kuwataka wavae kamera vifuani?

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
15,835
Reaction score
23,776
Jeshi la Polisi Tanzania, liliagizwa na Makamu wa Rais Hon Philip Mpango kuhakikisha wanavaa kamera ambazo zitaonyesha vitendo vyao vyote wawapo barabarani, hapa namaanisha Traffick mnamo 11-5-2024.

Traffick wamekuwa wakilalamikiwa sana, japo ni kama wanaonewa maana kwanza wanavaa nguo nyeupe kuashiria usafi lakini pia wanafanya kazi sehemu za wazi yaani barabarani kweupe na wamekuwa na utu sana.

Traffick wana utu kuliko kada yoyote kwakuwa kila asubuhi hu-simamisha daladala na madereva au kondakta hushuka na kwenda kusalimiana na traffik na kurudi wakikimbia, ni salamu.

Ikifika saa nne hukaa mbele ya mataa na kuvizia gari zinazopita na RED LIGHT, huu nao ni upendo kuwakumbusha watu.
Lakini pia wametumika na TARURA kukamata magari yaliyopigwa faini lakini hayalipi, ni weledi mzuri sana.

Traffik hawa pia ni wema maana wanawaonea huruma watu wa daladala, ambazo hazina taa, viti vimeoza, hayana rangi, yamegongwa na yanapita barabarani ila gari ndogo hata mchubuko tu unakamatwa!

Traffick pale Salander bridge kama unatokea mwenge kwenda kariakoo weekend lazma wasimamishe gari, huwapiti, wanakusalimia kwa upendo, tuendelee kuheshimu sheria za barabarani.

UPDATE:
Hili agizo limepuuziwa, Mheshimiwa Makamo wa Rais, umepewa tarifa kufuatia picha iliyoonekana maafisa polisi wakichukua chochote !

1.jpeg

11.jpeg

Pia soma=> Dkt. Mpango: Askari wa Barabarani wakianza kuvaa Kamera itapunguza Rushwa
 
Makamu wa Raisi alipotoa agizo hili aligawa hizo kamera kwa askari trafiki? Ametoa tamko la kisiasa, mkamshangilia akaondoka akiwacheka amewapata wajinga
 
Jeshi la Polisi Tanzania, liliagizwa na Makamu wa Rais Hon Philip Mpango kuhakikisha wanavaa kamera ambazo zitaonyesha vitendo vyao vyote wawapo barabarani, hapa namaanisha Traffick mnamo 11-5-2024.

Traffick wamekuwa wakilalamikiwa sana, japo ni kama wanaonewa maana kwanza wanavaa nguo nyeupe kuashiria usafi lakini pia wanafanya kazi sehemu za wazi yaani barabarani kweupe na wamekuwa na utu sana.

Traffick wana utu kuliko kada yoyote kwakuwa kila asubuhi hu-simamisha daladala na madereva au kondakta hushuka na kwenda kusalimiana na traffik na kurudi wakikimbia, ni salamu.

Ikifika saa nne hukaa mbele ya mataa na kuvizia gari zinazopita na RED LIGHT, huu nao ni upendo kuwakumbusha watu.
Lakini pia wametumika na TARURA kukamata magari yaliyopigwa faini lakini hayalipi, ni weledi mzuri sana.

Traffik hawa pia ni wema maana wanawaonea huruma watu wa daladala, ambazo hazina taa, viti vimeoza, hayana rangi, yamegongwa na yanapita barabarani ila gari ndogo hata mchubuko tu unakamatwa!

Traffick pale Salander bridge kama unatokea mwenge kwenda kariakoo weekend lazma wasimamishe gari, huwapiti, wanakusalimia kwa upendo, tuendelee kuheshimu sheria za barabarani.

UPDATE:
Hili agizo limepuuziwa, Mheshimiwa Makamo wa Rais, umepewa tarifa kufuatia picha iliyoonekana maafisa polisi wakichukua chochote !

View attachment 3050706

View attachment 3050707

Pia soma=> Dkt. Mpango: Askari wa Barabarani wakianza kuvaa Kamera itapunguza Rushwa

Jana kuna mmoja wa kike alinikamata maeneo ya mbezi beach kwa uonevu kabisa. Hawa wanastahili. Wamezidi tamaa
 
Back
Top Bottom