Hebel Mlagala
Senior Member
- Aug 4, 2012
- 134
- 49
Hivi karibuni nilimshuhudia Mchungaji Christopher Mtikila akimwambia askari aliye kuwa akitaka kumkamata kuwa hawezi kukamatwa na askari huyo kwakuwa cheo chake (huyo askari) ni kidogo na askari akatii.
Swali langu ni je askari anatakiwa kwenda kumkamata mtuhumiwa kwa kuzingatia cheo chake na hadhi ya mtuhumiwa. Na je mtuhumiwa ana haki ya kukataa kukamatwa na askari wa cheo cha chini?
Sasa mtu mwenye shahada mbili kwa mfano anatakiwa kukamatwa na askari wa cheo gani? Maana asije siku moja akatokea koplo kutaka kunikamata kumbe mimi nastahili kukamatwa na sajenti au meja au IGP mwenyewe!
Na je ni lazima askari ajitambulishe cheo chake wakati wa kumkamata mtuhumiwa au ni juu ya mtuhumiwa kujua cheo cha askri kwa kuangalia alama za vyeo au kumwuliza endapo atakuwa hajavaa sare?